»Udhibiti wa ugonjwa wa Kideri«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.accessagriculture.org/management-newcastle-disease

Muda: 

00:15:40
Imetengenezwa ndani: 
2020

Imetayarishwa na: 

NASFAM

Kuku hutoa nyama, mayai, mapato na mbolea kwa wakulima wengi. Lakini, kuku hukabiliwa magonjwa mengi. Kidera ni moja wapo ya magonjwa hatari ambao huua kuku sana ulimwenguni kwote. Pindi kuku wanapopata ugonjwa wa kideri, hakuna tiba na kuku wote kijijini wanakufa.

Dalili

Ugonjwa wa kideri huathiri akili ya kuku. Mabawa hupooza, kichwa na shingo hupinda, na kuku huonekana kuwa dahifu sana. Kinyesi chao huwa kimajimaji, rangi ya kijani ambacho hushikilia kwenye manyoya. Kuku huvimbea chini ya mabawa na kupiga chafya. Ugonjwa wa kideri husababishwa na virusi na husambazwa kupitia kwa kugusana moja kwa moja na kinyesi kutoka kwa kuku walioathiriwa, au na lishe, maji na mavazi ya binadamu yaliyo na virusi.

Kinga na udhibiti

Ugonjwa wa kideri unaweza kuzuiwa kwa njia za kudumisha usafi kama vile kutenganisha kuku wagonjwa, kuchinja na kuzika kuku walioathiriwa ili kuzuia ugonjwa kuenea. Tenganisha na karantisha kuku wapya waliotoka mahali tofauti.

Hakuna tiba ya ugonjwa wa kideri.

Chanjo

Chanjo ni njia bora ya kuzuia ugonjwa kwa sababu hakuna tiba ya ugonjwa huo. Chanjo zinafaa kuwekwa kwenye friji kwa viwango kati ya 2 ° C-8 ° C. Wakati wa kwenda shambani, chanjo kinafaa kusafirishwa ndani ya chombo kidogo kilicho na barafu au kama kimefungwa kwenye kitambaa kilichounyevu ndani ya ndoo iwapo hali ya joto sio juu sana.

Chanjo ya La Sota: Chupa moja ya chanjo ya La Sota huyeyushwa na lita 5 za maji, na inafaa kupewa kuku katika ya masaa 2 baada ya kuichanganya. Ili kunyunya chanjo vizuri, ongeza kijiko 1 cha unga wa maziwa kwenye mchanganyiko. Chupa ya chanjo inafaa kufunguliwa ndani ya maji ili kuhakikisha yoye imetumika. Mchanganyiko huo unaweza kumwagwa kwenye vyombo vya maji na kuwekwa katika sehemu tofauti. Unaweza pia kutumia sindano kuwapa kuku chanjo kupitia mdomoni moja kwa moja.

Chanjo ya i-2: Chanjo ya i-2 inapewa kwa kuweka tone moja ndani ya jicho la kuku. Chanjo hii haichanganywi kwa maji. Ili kuwa na ufanisi mzuri, chanjo hii inafaa kupewa katika masaa ya asubuhi. Kwa madhumuni ya usalama, dawa iliyobaki inafaa kuchomwa moto au kuzikwa.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:26Kuku hutoa nyama, mayai, mapato na mbolea kwa wakulima wengi.
00:2700:59Ugonjwa wa kideri ndio hua kuku wengi duniani
01:0002:34Ugonjwa wa kideri huathiri akili ya kuku. Mabawa hupooza, kichwa na shingo hupinda, na kuku huonekana kuwa dahifu sana. Kinyesi chao huwa kimajimaji, rangi ya kijani.
02:3502:58Husambazwa kupitia kwa kugusa kinyesi kutoka kwa kuku walioathiriwa, au na lishe, maji na mavazi ya binadamu yaliyo na virusi
02:5903:29Hakuna tiba ya ugonjwa wa kideri
03:3004:10Kuzuia: Tenganisha , kuchinja na kuzika kuku walioathiriwa, nakuchanja.
04:1106:20Kuchanja kuku
06:2109:50Uwezekano tofauti: chanjo kupitia vyombo vya maji, chanjo kupitia machoni.
09:5110:27Buy vaccinations for groups.Nunua chanjo kwa vikundi.
10:2811:31Usimamizi kwa kutumia chanjo: Chanjo lazima ifanyike kila mwezi 4.
11:3212:30Punguza hatari ya kuambukizwa kupitia hatua za usafi.
12:3113:00Dawa za asili haziponyi ugonjwa huo.
13:0115:40IIkiwa kuna maambukizo, kuku anafaa kuuawa na kuzikwa mara tu ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *