Mchele ni chakula kikuu kwa watu wengi, na uzalishaji wake hutoa ajira kwa watu wengi. Hata hivyo, uzalishaji wake huathiriwa na changamoto kadhaa.
Uzalishaji wa mchele kwa miaka mingi umekabiliwa na changamoto kama vile magugu. Magugu ni kikwazo kinachoathiri mavuno ya mchele. Udhibiti wa magugu unaweza kugawanywa katika aina mbili yaani, ule usiotumia kemikali na ule ambao kemikali kidogo hutumiwa.
Udhibiti usiotumia kemikali
Mbegu ambazo hazijaboreshwa huwa na mbegu za magugu ndani mwazo, na zikipandwa bila kuzichambua zinaweza kusambaza magugu shambani.
Maandalizi ya shamba hufanywa kwa kuandaa ardhi na kisha baada ya mvua ya kwanza, magugu huibuka na magugu haya huondolewa wakati wa kulima shamba mara ya pili kwa ajili ya kupanda.
Udhibiti wa kemikali
Udhibiti huu unahusisha matumizi ya dawa za kuua magugu kabla na baada ya magugu kuibuka. Unapotumia dawa za kuua magugu, nyunyuzia magugu yakiwa machanga, yaani wakati gugu limechipuka majani manne. Wakati magugu yanapovuka hatua ya majani manne, huwa umechelewa kutumia dawa za kuua magugu baada ya kuibuka.