Kilimo cha embe kinaathiriwa na magonjwa mbalimbali, jambo ambalo linapunguza uzalishaji.
Kilimo cha embe kinahitaji wakulima kujua changamoto zilizopo.
Madoa meusi ya bakteria hudhoofisha matawi na kusababisha matunda kudondoka.
Kutambua BBS
BBS hutambulika kwa uwepo wa madoa meusi, nyufa nyeusi, na nyufa zilizo na mikwaruzo kwenye majani, machipukizi na matawi yaliyokomaa.
BBS husababishwa na bakteria kutoka kwa miche iliyoambukizwa. Kiwango cha maambukizi ni kikubwa mwanzoni na mwishoni mwa msimu wa mvua.
BBS huingia kwenye mti kupitia sehemu za uharibifu na kuenea kupitia upepo hadi umbali wa 200m kila mwaka.
Udhibiti wa magonjwa
Ili kuzuia ugonjwa huo, wakulima wanahitaji kufanya kazi pamoja kama kikundi, kupanda miti shambani ili kujikinga na maambukizi.
Fanya utafiti, tumia miche isiyo na magonjwa, na ondoa sehemu zilizoambukizwa kutoka kwa mti.
Kagua shamba mara kwa mara, tunza maua kwanza, ondoa matunda yaliyoambukizwa na uyaharibu.
Usifanye kazi kwenye bustani wakati wa mvua. Ua viini kwa kutumia dawa kabla ya kutumia zana kwenye miti mingine.
Tumia viuakuvu. Ratiba ya kunyunyiza inategemea aina ya viuakuvu. Pia, fanya mashauriano.
Nyunyiza dawa za shaba, na za kimfumo kabla na baada ya maua kuchana, kwa muda wa wiki 2–3. Usinyunyize dawa wakati maua yanachana ili kuzuia kuharibu maua.
Sitisha kunyunyiza dawa wiki 3 kabla ya kuvuna. Usitumie dawa za kimfumo zaidi ya mara 3 kwa mwaka.
Badilisha matumizi ya viuakuvu vya kimiguso na vya kimfumo ili kuepuka ukinzani wa magonjwa.