Mabuu ya nzi wa matunda ni adui wa wakulima katika kilimo cha embe. Maembe yaliyoambukizwa hayawezi kuuzwa sokoni, na hivyo husababsiha hasara shambani.
Tatizo la kutumia kemikali kudhibiti nzi wa matunda ni kwamba dawa zinaweza kuua nzi wa matunda na baadhi ya wadudu wenye manufaa shambani. Kuvu ya kimapinduzi ambayo huua wadudu iitwayo metarhizium 69 imetengenezwa ili kudhibiti nzi wa matunda. Kifaa cha kuua wadudu kina vipengele viwili; unga wa metarhizium na kemikali za kuvutia wadudu.
Jinsi inavyofanya
Nzi wa matunda hutumiwa kusambaza unga wa kiuaji kwa nzi wengine. Nzi wa matunda dume huruka kwenye mtego ambao una unga huku akijaribu kufuata kemikali inayovutia wadudu. Katika mchakato huo, nzi huchukua kuvu, na wakati wanaondoka huisambaza kwa nzi wengine wa matunda.
Molasi huwekwa kwenye mtego kama chambo cha chakula ili kuvutia aina mbalimbali za wadudu dume na jike. Kisha mitego huning’inizwa katika mashamba ili kuvutia wadudu.
Faida
Mbinu za udhibiti wa kibayolojia ni za gharama nafuu, haziathiri mazingira, zina ufanisi bora na ni endelevu kwa matumizi ya muda mrefu.
Ni mbinu inayopendekezwa kwa sababu ni ya kibayolojia na inapunguza athari za dawa, na hivyo kulinda matunda na mboga.