Afya ya wanyama ni jambo muhimu ambalo huamua ubora na wingi wa bidhaa za wanyama.
Kwa vile ufanisi wa chanjo ya virusi hutegemea uwezo wa mnyama kuitikia chanjo, uchanganyaji sahihi, utunzaji na utumiaji wa chanjo, ni muhimu kufanya mashauriano kutoka kwa daktari wa mifugo ili kuzuia magonjwa ya ng‘ombe.
Kushughulikia chanjo
Kwanza, linda chanjo dhidi ya mwanga wa jua, joto, au baridi kali na uihifadhi kulingana na mwelekeo sahihi. Hifadhia sindano kwenye jokofu, na uepuke kuchanja ng‘ombe ambae hajakauka au wakati kuna halijoto kali.
Changanya chupa 2 zilizopatikana kwenye sanduku ili kuamilisha kiambatanisho. Katika mchakato huo, tumia sindano mpya ili kuepuka kuchafua chanjo. Ingiza sindano kwenye chupa ya plastiki, pindua chupa ya glasi na uiweke juu ya chupa ya plastiki huku ukihakikisha kwamba sindano imeingia chupa zote mbile ili kuhamisha chanjo.
Baada ya kuhamisha chanjo, ondoa sindano kutoka kwa chupa ya plastiki na utikise kwa upole hadi chanjo itakapochanganyika kabisa. Usitikise sana kwani huku kunaweza kuharibu vijenzi vya chanjo. Ili kuepuka hilo, soma maagizo yaliyoandikwa kwenye chupa.
Shikilia bomba ya sindano na chupa kwa mkono mmoja na tumia mkono mwingine kuondoa kipimo cha chanjo unachohitaji. Kisha chomoa sindano kwenye chupa huku ukielekeza juu, poa chanjo kidogo ili kuondoa hewa yoyote kwenye bomba au sindano, na hivyo kuhakikisha kipimo sahihi. Funga mnyama vizuri wakati wa kumdunga. Kwa sindano ya chini ya ngozi, tafuta sehemu safi ya mwili na tumia sindano mpya. Bainisha sehemu sahihi pa kudunga sindano. Kisha ingiza chanjo, na uondoe sindano huku ukiachilia ngozi.
Baada ya kuchanja, safisha sindano kwa kutumia maji ya moto na usitumie dawa za kuua viini. Kwa ufanisi, chanjo zote za virusi hai zinapaswa kutumika ndani ya saa moja baada ya kuchanganya, na sindano zinapaswa kutupwa ipaswavyo kulingana na kanuni.