»SLM10 uhuishaji asili wa ardhi kupitia wakulima«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.accessagriculture.org/slm10-managed-regeneration

Muda: 

00:06:58
Imetengenezwa ndani: 
2017

Imetayarishwa na: 

Countrywise Communication, CIS Vrije Universiteit Amsterdam

Uharibifu wa ardhi huleta tufani za vumbi zinazosababisha jangwa. Upandaji wa miti unaweza kutumika kama njia ya kupunguza athari za jangwa.

Kuanzisha miradi ya upandaji wa miti aina za kigeni kama vile mikaratusi na mipaina haifanyi vizuri katika maeneo ya ukame. Miti ambayo inaweza kustahimili na kuishi katika maeneo kame ni miti ya asili ambayo hutunzwa na wakulima.

Uhuishaji

Uhuishaji asili wa ardhi kupitia wakulima hufanywa kwa kuchagua miti iliyo na mashina ambayo yamenawiri zaidi na hivyo kusaidia miti hiyo kukua vyema ili kuhukumu aina bora ya uhuishaji. Hii inahitaji uzoefu pamoja na maarifa.

Miti yenye nguvu zaidi ambayo imebaki kwa miaka kadha huchaguliwa na kukatwa kwa mashina. Baadaye, miti michanga huchipuka kutoka kwenye mashina ikipata maji.

Umuhimu wa miti

Miti huzuia mmomonyoko wa ardhi unaosababishwa na upepo na maji. Miti huboresha muundo wa udongo kwa hivyo kurejesha rutuba ya udongo. Hii huruhusu kutekeleza kilimo endelevu.

Miti ya asili pia inaweza kutumika kama kuni wakati wa ukame, lakini itakua tena wakati mvua itakapoanza kunyesha.

Miti husaidia kustahimili mabadiliko ya hali ya hewa.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:40Uharibifu wa ardhi huleta tufani za vumbi zinazosababisha jangwa
0o:4101:48Upandaji wa miti unaweza kutumika kama njia ya kupunguza athari za jangwa.
01:4903 :07Uhuishaji asili wa ardhi kupitia wakulima hufanywa kwa kuchagua miti iliyo na mashina thabiti zaidi
03:0803:40Tambua aina ya miti unayopenda kupanda.
03:4104:45Kata mashina ya miti ili kuwezesha miti michanga kuchipuka.
04:4605:48Miti huboresha muundo wa udong, rutuba ya udongo na hivyo kusababisha kilimo endelevu. Panda aina tofauti za miti.
05:4906:24Miti husaidia kustahimili mabadiliko ya hali ya hewa.
06:2506:58Muhtasari

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *