»SLM06 Mashimo ya upandaji ya zaï«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.accessagriculture.org/slm06-zai-planting-pits

Muda: 

00:07:06
Imetengenezwa ndani: 
2017

Imetayarishwa na: 

Countrywise Communication, CIS Vrije Universiteit Amsterdam

Maji ya mvua yanayotiririka yanaweza kubadilishwa kuwa muhimu yakivunwa. Hii inaweza kufanywa kupitia mashimo ya upandaji ya Zai, ambayo hutumiwa kupokea mtiririko wa maji juu ya ardhi.

Mashimo ya Zai huchimbwa kwa mkono na jembe: yakiwa na kipenyo cha 25cm, kina cha 20cm, na muachano wa 90cm kwa kila mwelekeo. Udongo uliochimbuliwa huwekwa chini ya mteremko wa shimo.

Mbolea ozo huwekwa kwa usahihi kwenye mashimo ya zai kabla ya kupanda mtama au mawele. Kwa hivyo mvua inaponyesha, unyevu na virutubisho hujikusanyia haswa vinapohitajika.

Faida za mashimo ya Zai

Mbolea oza na mbolea ya kikaboni inayowekwa kwenye mashimo ya zai hutumika vizuri. Nafaka, kunde na mabaki ya mazao hutoa chakula kwa mifugo. Mashimo huongezwa na mistari ya mawe ambayo huwezesha udongo uliomomonyoka kujikusanyia katika Zai.

Zai hupanua mavuno na husaidia kuboresha hali ya ukame na jangwa kwa kupokea na kuhifadhi mtiririko wa maji. Miti pia hupandwa kwenye mashimo ya zai kama vile mishita ambayo yanaweza kutumika kama matandazo

Kuandaa mashimo ya Zai

Mashimo hutengenezwa kwa kutumia jembe liyoboreshwa ambayo huvutwa na farasi ili kufungua mistari. Reki iliyoboreshwa huvutwa kwa pembemraba ili kuonyesha mahali pa kutengeneza shimo la zai. Kisha mashimo huchimbwa, na mbolea huwekwa ndani. Njia hii hupunguza pembejeo ya wafanyikazi.

Nchi kama vile Burkina Faso na Niger hutumia njia ya mashimo ya zai.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:45Maji ya mvua yanayotiririka yanaweza kubadilishwa kuwa muhimu yakivunwa.
00:4401:05Mashimo ya upandaji ya Zai hutumiwa kupokea mtiririko wa maji juu ya ardhi.
01:0601:33Mashimo ya Zai huchimbwa kwa mkono na jembe: yakiwa na kipenyo cha 25cm, kina cha 20cm, na muachano wa 90cm kwa kila mwelekeo.
01:3401:50Mbolea ozo huwekwa kwa usahihi kwenye mashimo ya zai kabla ya kupanda mimea.
01:5102:25Mbolea oza na mbolea ya kikaboni inayowekwa kwenye mashimo ya zai hutumika vizuri. Mabaki ya mazao hutoa chakula kwa mifugo
02:2603:15Mashimo huongezwa na mistari ya mawe ambayo huwezesha udongo uliomomonyoka kujikusanya, na hivyo kuongeza mazao.
03:1604:13Zai huboresha hali ya ukame na jangwa. Kwa miti ambayo hupandwa kwenye mashimo ya zai, majani yake yanaweza kutumika kama matandazo
04:1404:44Mashimo ya zai hutengenezwa kwa kutumia mashine ili kupunguza pembejeo la wafanyikazi
04:4506:08Nchi kama vile Burkina Faso na Niger hutumia njia ya mashimo ya zai.
06:0907:06Muhtasari.

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *