»Shughuli za kuzaa ndama katika ufugaji wa ng‘ombe wa maziwa«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=yo5DIxkHV1s

Muda: 

00:10:46
Imetengenezwa ndani: 
2016

Imetayarishwa na: 

Digital Agriculture
Related videos

Kwa kawaida ng’ombe huzaa baada ya miezi 9 ya ujauzito. Hata hivyo, kuna taratibu kadhaa zinazopaswa kutekelezwa na kuzingatiwa na wafugaji wakati wa kuzaa ndama.

Kwa hiyo, ni muhimu kuwahamisha ng‘ombe wajawazito kwenye zizi lisilo na utelezi wiki 2 kabla ya kuzaa. Zizi linapaswa kusafishwa na kuuliwa viini vinavyosababisha magonjwa. Inashauriwa pia kutosumbua ng‘ombe anayezaa isipokuwa usaidizi unahitajika kwani huku kunanaweza kuzuia uwezo wa mnyama kuzaa vizuri.

Hatua zinazohitajika

Baada ya kuzaa, ruhusu mama kumramba ndama aliyezaliwa ili kuboresha mzunguko wa damu.

Pia ondoa kamasi puani na masikioni mara moja ili kuzuia kuziba na kuwezesha ndama kupumua. Safisha ndama aliyezaliwa kwa kitambaa safi na mabua ya mpunga yaliyokatwakatwa ili kumkausha ndama.

Funga kitovu 2.5cm kutoka kwa mwili wake na kata kitovu 1cm chini ya mfungo. Kisha chovya sehemu ya kitovu iliyokatwa kwenye mmumunyo

wa viuavijasumu ili kudhibiti maambukizi.

Mpime ndama aliyezaliwa ili kutambua uzani wake, na kumpa ndama maziwa ya kwanza ndani ya saa 1 baada ya kuzaliwa. Maziwa ya kwanza kutoa virutubisho na kingamwili kwa ndama mchanga.

Tenganisha ndama wachanga kutoka kwa mama na uwatolee huduma ya kutosha ili kuzuia vifo vya ndama.

Uwapo kuna changamoto katika kuzaa, mpe mnyama usaidizi ufaao. Hatimaye, ondoa kondo la nyuma linaposhindwa kushuka kiasili ndani ya saa 8.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0001:10Wahamishe ng‘ombe wajawazito kwenye zizi lisilo na utelezi wiki 2 kabla ya kuzaa. Zizi linapaswa kusafishwa na kuuliwa viini.
01:1102:41Usimsumbue ng‘ombe anayezaa isipokuwa usaidizi unahitajika
02:4203:25Baada ya kuzaa, ruhusu mama kumramba ndama aliyezaliwa.
03:2603:55Ondoa kamasi puani na masikioni mwa ndama mara moja
03:5605:30Safisha ndama aliyezaliwa kwa kitambaa safi na mabua ya mpunga yaliyokatwakatwa
05:3106:33Funga kitovu 2.5cm kutoka kwa mwili wake na kata kitovu 1cm chini ya mfungo.
06:3406:56Chovya sehemu ya kitovu iliyokatwa kwenye mmumunyo wa viuavijasumu
06:5708:15Mpime ndama aliyezaliwa na kumpa ndama maziwa ya kwanza ndani ya saa 1 baada ya kuzaliwa.
08:1608:32Tenganisha ndama wachanga kutoka kwa mama na uwatolee huduma ya kutosha.
08:3309:38Mpe mnyama usaidizi ufaao.
09:3910:46Ondoa kondo la nyuma linaposhindwa kushuka kiasili ndani ya saa 8.

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *