Kwa kuwa ni biashara yenye faida kubwa, ubora na wingi wa bidhaa zinazopatikana kwa ufugaji wa mbuzi aina ya bangal hubainishwa na mbinu ya uzalishaji inayotumika.
Mbuzi aina ya bengal hutoka nchini Bangladesh na ufugaji wao ni biashara yenye faida kubwa. Mbuzi hawa ni chanzo kizuri cha nyama, na pia huzaa watoto wengi, yaani mara mbili kwa mwaka.
Usimamizi wa mbuzi
Mbuzi aina ya bengal hustahimili hali ya hewa yoyote, na hivyo hufugwa sana. Ufugaji wa mbuzi ni chanzo kizuri cha kipato, ajira na huhitaji kibarua kidogo kwani mbuzi wa hawa wama mwili mdogo, na hivyo huhitaji makazi kidogo.
Vile vile, nafasi ya takriban futi 10 za mraba inahitajika kwa kila mbuzi. Kwa mbinu ya banda lililoinuliwa, unahitiaji futi 20–25 za mraba kwa kila mbuzi. Hakikisha kuna uingizaji mzuri wa hewa ndani ya banda, na pia jenga uzio kuzunguka banda ili kuwalinda mbuzi dhidi ya wanyama wawindaji. Hifadhi vyombo vyote vya kulishia na kunyweshea maji ndani ya chumba. Tengeneza vyumba tofauti ili kutenganisha mbuzi wa kuzaliana, wajawazito na wanaonyonyesha.
Banda lazima liwe na sakafu ya mbao, na liinuliwe kwa urefu wa futi 4–5 kutoka ardhini, na futi 6–8 kutoka kwa sakafu hadi paa. Sakafu lazima iwe na miachano kati ya mbao ili mkojo wa mbuzi utiririke chini kwa urahisi. Weka damani za plastiki kwenye madirisha ili kuwalinda mbuzi dhidi ya baridi kali. Weka mbuzi aliezaa na watoto katika sehemu maalum usiku katika wakati wa msimu wa kibaridi.
Safisha banda kila asubuhi. Tolea mbuzi lishe bora kwa ukuaji bora. Watolee maji safi, tunza dume bora kwa ajili ya kuzaliana kiasili. Tenganisha mbuzi wajawazito kabla ya kuzaa.
Watoto wanapaswa kuzaliwa katika sehemu kavu, na lazima wasafishwe baada ya kuzaliwa. Mpe mtoto maziwa ya kwanza saa chache baada ya kuzaliwa ili kuongeza kingamwili. Walishe watoto kwa kutumia njia bandia wakati maziwa ya mama hayatoshi.
Hatimaye, chanja mbuzi na uwe na uhusiano mzuri na daktari wa mifugo.