»Ratiba mpangilio wa kutunza mbegu za mpunga«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.accessagriculture.org/rice-seed-preservation

Muda: 

00:07:07
Imetengenezwa ndani: 
2016

Imetayarishwa na: 

Agro-Insight, CABI, Countrywise Communication, IRRI, RDA, TMSS

Wakulima wengi huhifadhi mbegu zao za mpunga kwa upanzi wa mwaka unaofuata. Lakini wanafaa kuhifadhi mbegu hizo vizuri ili ziwe na afya, pamoja na ubora wa hali ya juu.

Mbegu ni hai. Ili kupata mavuno mazuri, panda mbegu zenye afya. Hewa na unyevu huharibu mbegu. Ikiwa mbegu hazijahifadhiwa kwa njia sahihi huwa laini, na unyevu na, kwa hivyo zinaweza kushambuliwa na magonjwa na wadudu. Ukiweka chombo chini kwenye sakafu, mbegu hupata unyevu kutoka kwa udongo, kuva, na ukungu.

Kuhifadhi mbegu za mpunga

Chagua na uvune wimbi nzuri. Pura na uikaushe. Ili kujua kama mbegu imekauka,unaweza kuiuma kwa meno. Osha, safisha na kausha chombo kabla ya kukitumia kuhifadhi mbegu, ili kuhakikisha kwamba hakina wadudu na mayai yao. Unaweza kuzihifadhi mbegu kwenye vyombo vya plastiki, mikebe na mapipa.

Unaweza pia kuhifadhi mbegu hizo kwenye nyungu, maadamu utaziweka dhidi ya upenyezaji wa hewa. Hewa inaweza kupenyeza sio tu kupitia kifuniko bali hata kupitia nyufwa au mashimo madogo yaliyo katika nyungu. Kwa kuweka vanish au lami, unaweza kuondoa mashimo madogo. Pata rangi ya uchoraji kutoka kwa duka la vifaa, au tumia varnish au lami. Unaweza pia kutumia mafuta ya kupikia badala ya rangi. Hakikisha kupaka rangi kwote ndani na nje ya nyungu.

Wanawake wengine huweka mishumaa inayowaka ndani ya chombo na kukifunika. Mshumaa utawaka hadi oxygen(oksijeni)itakapoisha. Wadudu wanahitaji hewa kwa kupumua na kuzaa, kwa maana kuwasha mshumaa wadudu wote ndani ya chombo watafariki.

Jaza chombo na mbegu kavu hadi pumoni. Ikiwa hauna mpunga wa kutosha unaweza pia kutumia mchanga uliokaushwa kujaza akiba. Sasa ongeza majani ya bishkatali kavu, mwarobaini au majani ya tumbaku, ili kudhibiti wadudu. Funga kifuniko vizuri, ili hewa isiingie ndani.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:20Utangulizi
00:2100:32Mbegu ni hai
00:3300:52Wakulima wengi huhifadhi mbegu zao za mpunga kwa upanzi wa mwaka unaofuata
00:5301:06Lazima uhifadhi mpunga vizuri ili uwe na afya.
01:0702:03Ikiwa mbegu hazijahifadhiwa kwa njia sahihi huwa laini, na unyevu na, kwa hivyo zinaweza kushambuliwa na magonjwa na wadudu.
02:0402:16Chagua na uvune wimbi nzuri. Pura na kuzikaush
02:1702:25Ili kujua kama mbegu imekauka,unaweza kuiuma kwa meno
02:2602:38Osha, safisha na kausha chombo kabla ya kukitumia kuhifadhi mbegu, ili kuhakikisha kwamba hakina wadudu na mayai yao
02:3902:44Unaweza kuzihifadhi mbegu kwenye vyombo vya plastiki, mikebe na mapipa.
02:4502:57Unaweza pia kuhifadhi mbegu hizo kwenye nyungu, maadamu utaziweka dhidi ya upenyezaji wa hewa.
02:5803:34Kwa kuweka rangi ama ya mafuta ya kupikia , unaweza kuondoa mashimo madogo katika nyungu.
03:3504:04Wanawake wengine huweka mishumaa inayowaka ndani ya chombo na kukifunika
04:0504:16Jaza chombo na mbegu kavu hadi pumoni
04:1704:28Ikiwa hauna mpunga wa kutosha unaweza pia kutumia mchanga uliokaushwa kujaza akiba.
04:2904:47Sasa ongeza majani ya bishkatali kavu, mwarobaini au majani ya tumbaku, ili kudhibiti wadudu.
04:4805:12Ukiweka chombo chini kwenye sakafu, mbegu hupata unyevu kutoka kwa udongo, kuva, na ukungu.
05:1306:31Muhtasari
06:3207:07Credits

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *