Kupitia kujifunza usimamizi na ufugaji bora wa kuku wa kienyeji, wafugaji hupata pesa.
Kwa kutumia mshumaa, shikilia ncha kubwa ya yai dhidi ya mwanga wa mshumaa ili kuona mtandao wa mishipa ya damu na ukuaji wa yai. Kwa vifaranga 40 – 50 banda la kuku linapaswa kuwa na urefu wa futi 6 na upana wa futi 4, na urefu wa futi 2.75 kwenda juu. Kuku wazima wanahitaji gramu 50 – 60 za chakula kila siku.
Mbinu za ufugaji
Tengeneza banda lililo na vyumba vidogo vya maji, mayai na malisho kwani kuku wanaotaga hawawezi kuacha mayai kwa ajili ya chakula na maji. Tumia mshumaa kutambua mayai yanayokua na kuyatenganisha na mayai yasiyokua. Tenganisha vifaranga mama na kuku wengine wazima, wiki baada ya mayai kuanguliwa ili kuwezesha mama kutaga mayai tena kwa urahisi. Pia hakikisha kuna uingizaji wa hewa ya kutosha katika banda la kuku, na ulinzi dhidi ya wanyama waharibifu.
Banda la Kuku
Daima jenga banda la kuku chini ya mti ili kuepuka jua moja kwa moja. Unapaswa kuchanja kuku dhidi ya magonjwa kadhaa kwa kushauriana na wakala wa ugani juu ya vyanzo vya chanjo vinavyoaminika. walishe kuku chakula bora ili waweze kuwa na afya nzuri. Jitengenezee vyakula vya kuku kwa kuchanganya mchele, maganda ya mayai, samaki wakavu, maganda ya konokono, chumvi na majani. Fuatilia kwa ukamilifu gharama za pembejeo, na mapato ili kujua kama unapata faida au hasara.