»Nyavu (chandarua) dhidi ya wadudu katika kitalu«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.accessagriculture.org/insect-nets-seedbeds

Muda: 

00:11:35
Imetengenezwa ndani: 
2016

Imetayarishwa na: 

Agro-Insight

Miche ya mboga huhitaji utunzaji maalum kwa sababu hushambuliwa sana na wadudu. Viuawadudu sio tu ghali, lakini pia ni hatari kwa afya ya watu. Kwa hivyo, ni bora kutumia nyavu (chandarua) za wadudu ili kupunguza utumizi wa viuawadudu.

Wadudu waharibifu wa mazao ni; konokono, na panzi ambao hula na kukata mimea, viwavi ambavyo hushambulia nyanya, kabichi na pilipili. Nzi weupe hufyonza maji ya mimea, na hivyo kuchelewesha ukuaji wa mmea na kusambaza virusi.

Kuweka wavu (chandarua)

Unaweza kununua wavu iliyotengenezwa tayari au kujitengenezea yako. Wakati wa kutengeneza, ongeza 1m kwa urefu na upana wa kitalu ili kujua kiasi unachohitaji.

Baada ya kupata wavu, tumia vifaa vinavyopatikana kama vile matawi, vijiti ili kustahimili wavu. Vikate vijiti kwa urefu wa kutosha ili wavu iweze kupita nusu mita juu ya udongo.

Weka vijiti kwa pande zote za kitalu na uondoe sehemu zilizochongeka. Funika kitalu kwa kutumia matandazo, kisha weka wavu, na pia weka udongo kuzunguka wavu ili kuweza kuifunga vizuri.

Baada ya siku 8–9, fungua wavu na uondoe matandazo wakati miche inapoanza kuota. Baada ya hapo, unafaa kuweka majani kando kando ili kuipa kivuli ikiwa jua ni kali.

Wakati unapokaribia kupandikiza miche, ondoa wavu.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0001:39Miche za mboga huvamiwa sana na wadudu na huhitaji uangalifu maalum.
01:4002:15Viuawadudu sio tu ghali, lakini pia ni hatari kwa afya ya watu. Kwa hivyo, ni bora kutumia nyavu.
02:1604:38Konokono, panzi, na viwavi hushambulia na kula miche.
04:3905:39Nzi weupe hufyonza utomvi wa mimea, na hivyo kuchelewesha ukuaji wa mmea na kusambaza magonjwa.
05:4006:22Kuweka wavu (chandarua)
06:2307:25Ongeza 1m kwa urefu na upana wa kitalu ili kujua kiasi unachohitaji
07:2608:16Tumia vifaa vinavyopatikana kama vile matawi, vijiti ili kustahimili wavu
08:1708:24Funika kitalu kwa matandazo, kisha weka wavu.
08:2508:39Weka udongo kuzunguka wavu
08:4008:59Fungua wavu na uondoe matandazo wakati miche inapoanza kuota
09:0009:19Weka majani ya mnazi kando kando ili kuipa kivuli ikiwa jua ni kali
09:2009:39Tunza wavu vizuri ili kuitumia msimu ujao.
09:4011:35Muhtasari

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *