Uzalishaji wa maziwa nchini Kenya unakadiriwa kuwa kati ya kilo 1300 hadi 4575 kila mwaka kwa kila ng’ombe kutoka kwa aina mbalimbali za ng’ombe wa maziwa.
Tofauti katika uzalishaji huchangiwa na upatikanaji wa milisho bora, aina ya ng’ombe, na mifumo ya uzalishaji. Nyasi aina ya brachiaria ni ya asili barani Afrik,a lakini hukuzwa katika ulimowenguni kote. Nyasi hiyo iliboreshwa hivi majuzi na kuwa aina bora zaidi nchini Kenya. Aina ya brachiaria mulato 2 hukua haraka na hustawi katika muda wa miezi mitatu, na inaweza kuvunwa kwa mara ya kwanza.
Kulisha ng’ombe wa maziwa
Ng’ombe wa maziwa hula asilimia 3% ya chakula ambacho kinalinganishwa na uzito wa mwili wake. Ng’ombe wa maziwa wenye uzito wa kilo 60 –100 kg hula kilo 2.2 ya chakula kinachotengenezwa na kuuzwa madukani, na gramu 100 –150 ya chakula cha nyongeza.
Utumiaji wa malisho bora husababisha uzalishaji bora na hupunguza gharama kwa kuwa malisho huchangia hadi 70% ya gharama za uzalishaji katika ufugaji wa ng’ombe wa maziwa.
Masharti ya ukuaji wa nyasi
Nyasi ya brachiaria hutoa mbegu, tofauti na napier. Nyasi hukua hadi mita 1.5 juu katika udongo bora na hali ya hewa bora. Masharti ni; maeneo yenye mvua zaidi ya 700 mm kwa mwaka na wastani wa joto usiozidi 19°C.
Nyasi hukua vizuri kwenye udongo wowote isipokuwa udongo wa mfinyanzi. Pia hukua vizuri katika maeneo yasiyozidi 800 m – 1800 m chini ya usawa wa bahari. Nyasi ya brachiaria ina asilimia 18% ya protini ghafi.
Faida
Mavuno ya brachiaria ni kati ya tani 18–20 za malisho kwa ekari. Nyasi ya brachiaria inapokaushwa na kufungwa kwenye maraoboto, hutoa tani 8.5-tani 10. Nyasi brachiaria hupendelewa kwa manufaa yake ya kutoa mavuno mengi kwa mwaka.
Nyasi ya brachiaria pia ina kiwango cha juu cha nyuzinyuzi na huongeza uzalishaji wa maziwa kwa 40%, hustahimili ukame kwa miezi 5–6. Inaweza pia kustahimili udongo wa alkali na tindikali, na ni sugu kwa wadudu na magonjwa.