Nguruwe waliokomaa huathiriwa na joto huku nguruwe wachanga wakiathiriwa ubaridi. Udibiti wa joto husaidia kuongeza ukuaji wa nguruwe.
Aina ya large white ni moja wapo ya nguruwe wanaofugwa sana, na hutumiwa sana katika kuzaliana. Aina ya landrace ina uwezo wa kuboresha aina nyingine za nguruwe. Aina hii ina nyama bora kwa sababu ya misuli yake mikubwa. Pia hukomaa mapema, hukua haraka, na hupata uzito mkubwa wakati wa kumwachisha kunyonya.
Ufugaji wa nguruwe
Wana nguruwe huzaliwa na jozi ya meno makali ambayo yanaweza kuathiri matiti ya nguruwe mama. Wanaumiza wenzi wao na kusababsiha majeraha usoni wakati wakupigana, na wanaweza pia kuuma mikia yao na kusababisha maambukizo. Punguza meno ya nguruwe wachanga ili kuzuia hili.
Upunguzaji wa mkia hufanywa ili kupunguza matukio ya nguruwe kujiuma mikia na kula wenzao. Katika shughuli hii, tumia mkasi mkali ili kupunguza maumivu na hatari ya maambukizi.
Kulisha na kuzaa
Nguruwe wachanga hulishwa peleti kwa muda wa siku 45 hadi 60 ili kufanya kama nyongeza kwa maziwa kutoka kwa nguruwe mama. Nguruwe huhitaji protini kwa ukuaji, uzalishaji wa maziwa, utunzaji wa mwili na ukuaji wa kijinsia.
Ukuaji wa kijinsia hupimwa kwa uwezo wa nguruwe jike kupata joto katika miezi saba na kubeba mimba muda kamili na kuzaa angalau watoto 10 wenye afya nzuri.
Chanzo cha maji
Maji yanapaswa kuwa baridi, safi na ya kutosha kwani nguruwe hunywa maji mengi. Mirija ya maji inapaswa kuzikwa ardhini ili kudumisha ubaridi.
Mrija ya vihori vya maji inafaa kuchunguzwa ili kuhakikisha kwamba maji yanatiririka ipaswavyo.
Nguruwe wanaonyonyesha wana hitaji kubwa la maji kwa sababu ya uzalishaji wa maziwa.