Nguruwe wa umri wote hushambuliwa na magonjwa ya matumbo na kuhara. Kuwa na mpango wa afya ya mifugo utasaidia kupunguza magonjwa shambani.
Magonjwa ni changamoto mkubwa wa gharama katika ufugaji, na husababisha hasara kubwa. Ugonjwa wa upele au ukurutu hufanya ngozi ya nguruwe kuwa dhaifu. Ili kudhibiti magonjwa, osha na kukausha banda la nguruwe mara moja kwa mwezi. Ikiwa nguruwe amefungiwa bandani, weka shimo au mfereji nyuma ya zizi ili kuruhusu mkojo kuondoka. Safisha miguu yako unapotoka banda lingine ili kuzuia kueneza magonjwa.
Faida za kuua viini
Dawa za kuua viini hutumika kuua vijidudu ambavyo husababisha magonjwa. Dawa hizi hufanya kama sumu.
Dawa za Antiseptics huzuia bakteria na hutumiwa kusafisha ngozi au vidonda.
Mabua ya mmea wa ngano hutumiwa kama matandiko bandani. Dumisha usafi bandani.
Faida za ufugaji wa nguruwe
Kiasi kidogo cha fedha hutumika kuanzisha ufugaji wa nguruwe. Nguruwe huzaa zaidi ya watoto 10 kwa wakati mmoja. Chakula cha nguruwe kinapaswa kuwa cha ubora wa juu ili kuhakikisha nguruwe wanafikia uzito unaohitajika. Wiki tatu baada ya kuzaa mkulima anafaa ahasi nguruwe dume wote, na kuanza kuwalisha chakula kigumu.
Wakulima wanapaswa kuwapa nguruwe wa kike chakula bora cha kutosha kwani watoto hupata mahitaji yao yote ya lishe kutoka kwa maziwa ya mama zao.