Umwagiliaji kwa njia ya mafuriko husababisha uongezeka la kiwango cha maji, kutwama kwa maji na ongezeko la chumvi kwenye udongo wa juu.
Mafuriko yanapotokea, mizizi hushindwa kunyonya madini na virutubisho kutoka kwenye udongo, na hivyo kuathiri afya ya jumla ya zao hilo. Upitishaji mzuri wa maji ni muhimu hasa katika udongo wa mfinyanzi. Ili kuzuia maji kutwama, ardhi inaweza kusawazishwa japokuwa wakati mwingine hata hii haitoshi.
Kutengeneza vitalu vilivyoinuliwa
Vitalu vilivyoinuliwa lazima viwe na urefu wa cm 20 hadi 30, upana wa 80 hadi 100 na 500 hadi 100 m kutegemeana na mteremko. Kutengeneza vitalu vilivyoinuliwa huokoa maji, huongeza mavuno na kuokoa muda na gharama za umwagiliaji kwa vile maji huelekezwa tu kwenye shamba.
Mashine zinaweza kutumika kuandaa vitalu vilivyoinuliwa vya ukubwa unaohitajika. Mashine hizo zinaweza pia kutengeneza vitalu, na pia kupanda kwa wakati mmoja.
Kupanda kwenye vitalu
Faida ya vitalu vilivyoinuliwa ni kwamba ikiwa kuna mvua kubwa, maji hayatafurika juu ya vitalu vilivyoinuliwa ili kuharibu mazao.
Kwa maharage ya fava, weka mbegu moja kila baada ya 20cm na panda katika safu 3. Kwa ngano, pia weka mbegu kwenye safu kwa muachano wa 15cm kati ya safu.
Mara tu baada ya kupanda, furika shamba zima, lakini kwa umwagiliaji unaofuata, jaza tu mitaro.
Unaweza kutumia vitalu vyako kwa misimu 2 hadi 3 ya upanzi ikiwa hutaki kulima shamba lako kila msimu.