Uthibitisho wa kimataifa wa kikaboni unaweza kuwa wa gharama kubwa na wakulima hawawezi kumudu gharama hizo. Katika nchi nyingi, mfumo wa udhamini shirikishi umetokea kama njia mbadala ya uthibitisho hasa kwa wakulima wadogo.
Njia ya utekelezaji
Ingawa mifumo ya udhamini shirikishi inaundwa ndani ya nchi na inatofautiana kutoka nchi moja hadi nyingine, yote yana kitu kimoja sawa. Wakulima ndani ya kikundi hujipanga katika kamati ambayo hutembelea mashamba ya kila mmoja ili kuhakikisha kuwa mazao yanazalishwa kwa njia ya kikaboni.
Wakati kikundi kinapokuwa kipya, wanachama wanaweza kutembeleana mara chache ndani ya msimu ili kuhakikisha kuwa wanaendelea na kilimo cha kikaboni.
Wanachama wawili au watatu wa mfumo wa dhamana kawaida hutosha kumtembelea mwanachama na kufanya ukaguzi. Wakati wa ukaguzi, taarifa kuhusu mazao yanayolimwa, mbolea ya kibaiolojia inayotumika na jinsi wadudu waharibifu wanavyodhibitiwa shambani hukusanywa na kujazwa katika fomu.
Mwishoni mwa ziara, kamati husaini fomu na kuihifadhi kwa kumbukumbu.
Baada ya muda, mashamba yaliyotembelewa pia yanaanza kubadilishana maarifa kwa wakulima wengine.
Inspekta mzuri ni yule ambaye hushauri. Huwa anasikiliza maswala ya wakulima kwa makini na kisha hutoa ushauri wa kiufundi.
Mpito wa kilimo kiikolojia
Malengo ya mfumo shirikishi wa dhamana ni kuwezesha uzalishaji wa chakula salama na kurejesha mazingira.
Mwaka wa kwanza wakati mkulima anabadilika kutoka kwa kilimo cha kawaida kwenda kwa kikaboni, hupata cheti ambacho huonyesha kwamba yuko katika kipindi cha mpito na anajitolea kuboresha kilimo chake cha kikaboni.
Baada ya kutimiza hilo, hupata cheti cha kikaboni ambacho kinampa mkulima thamani sokoni.
Ili kuboresha mauzo yako, ni muhimu kuruhusu jamii kuelewa lebo ya mfumo wa dhamana shirikishi. Lebo inaweza kutumika kwenye kufungasha matunda na mboga.
Wakulima wa kikaboni wanaweza kuomba bei zaidi kidogo kuliko wakulima wa kawaida.