Mahindi huathiriwa sana na wadudu kama vile viwavi wanao toboa shina la mmea. Hii husababisha mazao duni. Mfumo wa vuta-sukuma una kipengele cha kutekeleza usimamizi jumuishi wa wadudu.
Viwavi hutaga mayai kwenye majani ambayo huanguliwa kuwa mabuu kwa angalau siku 4–8. Viwavi vinavyotokea huanza kula ma kuharibu majani. Viwavi ni rangi nyeupe au hudhurungi, na wana vichwa vilivyo na rangi ya kahawia, na misatri 4 mirefu kwa miili yao. Viwavi huingia ndani ya mmea ili kulisha na hivyo kuuharibu. Viwavi hubadilika na kuwa kifukofuko baada ya wiki 2 – 4, na mwishowe huwa nondo kwa siku 2 hadi 12. Nondo hushughulika wakati wa usiku, na hupumzika kwenye mimea wakati wa mchana.
Kudhibiti wa viwavi wanaotoboa mashina
Katika mfumo wa vuta-sukuma, panda mimea kama vile desmodium ambayo hufukuza nondo katika mahindi, pamoja na kudhibiti magugu. Mimea hiyo baadaye hulishwa mifugo. Panda mahindi kwa muachano wa 2 ft kati ya safu, na desmodium katikati ya safu za mahindi ili kutekeleza mbinu ya sukuma-vuta. Desmodium hutoa kemikali ambazo wadudu hawapendi. Kwa hivyo nondo hufukuzwa nje ya mahindi. Nje ya shamba la mahindi, panda nyasi za napia ambazo huvutia nondo kutoka kwa mahindi. Nondo hutaga mayai yao kwenye nyasi za napai.