»Mbolea minyoo ya maji maji: Dawa asili ya mimea «

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.accessagriculture.org/vermiwash-organic-tonic-crops

Muda: 

00:13:22
Imetengenezwa ndani: 
2020

Imetayarishwa na: 

Shanmuga Priya

Mbolea minyoo ya maji maji ni mbolea asili ambayo inaweza kuboresha rutuba ya udongo tena. Ni maji maji yanayokusanywa kutokana na maji yanayopitia kwenye mbolea ya mboji iliyotengenezwa na minyoo.

Mbolea hii ina vichocheo vya ukuaji, virutubisho ambavyo huhitajika na mimea katika viwango vidogo (virutubisho lishe), pamoja na virutubisho vivavyo huhitajika na mimea katika viwango vikubwa (virutubisho muhimu) kama vile nitrojeni, fosforasi na potasiamu. Mbolea hii huwekwa moja kwa moja kwa majani ya mimea ili kusababisha ukuaji wa haraka na pia gharama yake ni nafuu kuliko mbolea oza. Mbolea minyoo huongeza idadi ya viumbe hai wenye faida kwenye udongo ambao husaidia mmea kunawiri. Pia inaboresha mimea bila kudhuru mazingira. Husaidia mimea na udongo kustahimili magonjwa na mashambulio ya wadudu. Ikilinganishwa na mbolea za kemikali, mbolea hii huongeza mazao na kupunguza gharama.

Kutengeneza mbolea minyoo ya majimaji

Mbolea minyoo ya maji maji hutengenezwa kwa pipa la plastiki la lita 100, na bomba. Kuzuia bomba kuziba, tumia vipande vidogo vya chandarua au kitambaa cha pamba kama kichungi. Weka pipa katika eneo lenye kivuli kwa sababu viumbe hai vyenye faida vilivyo kwenye mbolea minyoo ya maji maji vitakufa kwa joto kali. Jaza pipa na cm 10 hadi 15 ya majani makavu, kisha ongeza kiasi sawiya cha majani ya mpunga, na kilo 5 hadi 10 ya samadi ya ng‘ombe iliyooza. Ongeza 2kg ambazo ni sawa na minyoo 2000 ndani ya pipa. Ongeza lita 2 hadi 4 za maji kwa upole ili kuepuka kuwadhuru minyoo. Funika pipa kwa kitambaa ili kuepuka minyoo kushambuliwa na mchwa.

Mchanganyiko na usimamizi

Baada ya siku 10, mbolea minyoo ya maji maji huanza hujitengeneza kwenye pipa. Kila siku, unaweza kukusanya lita 1 hadi 3 za mbolea minyoo ya maji maji kutumia bomba. Mbolea minyoo ya maji maji ambayo ni bora ina rangi ya hudhurungi na inaweza kuhifadhiwa hadi miezi 6. Ongeza lita 1 ya mbolea minyoo ya maji maji kwa lita 10 za maji. Mkojo unaweza pia kuongezwa kwa mbolea minyoo ya maji maji kwa sababu mkojo hufanya kama dawa ya kuvu. Nyunyiza mchanganyiko wa mbolea minyoo ya maji maji wakati mimea inapochana maua. Nyunyiza mimea asubuhi mapema au jioni ili kuepusha joto kuyeyusha mbolea.

Mbolea minyoo ya maji maji pia inaweza kutumika katika umwagiliaji wa matone. Unaweza pia kulowesha mizizi ya miche kwenye mbolea minyoo ya maji maji kabla ya kupandikiza miche, na hivyo mizizi itakuwa yenye nguvu na afya. . Mbolea minyoo ya maji maji inaweza kunyunyizwa kwenye udongo kabla ya kupandikiza miche ili kudhibiti wadudu.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0001:00Virtutubisho vya udongo kama vile zink na iyon huhitajika na mimea katika viwango vidogo. Kulima mimea katika udongo huo husababisha hupotezaji wa virutubisho vyake.
01:0102:18Mbole hii ni maji maji yanayokusanywa kutokana na maji yanayopitia kwenye mbolea ya mboji iliyotengenezwa na minyoo. Mbolea hii huwekwa moja kwa moja kwa majani ya mimea
02:1903:15Mbolea minyoo huongeza idadi ya viumbe hai wenye faida kwenye udongo
03:1603:52Hutengenezwa kwa pipa la plastiki la lita 100, na bomba. Tumia vipande vidogo vya chandarua au kitambaa cha pamba kama kichungi. Weka pipa katika eneo lenye kivuli
03:5304:32Jaza pipa na cm 10 hadi 15 ya majani makavu, na majani ya mpunga. Ongeza samadi ya ng‘ombe iliyooza, na minyoo kisha umwagilie maji.
04:3305:25Epuka kusindilia nyenzo ulizoweka kwenye pipa. Ongeza lita 2 hadi 4 za maji kwa upole huku ukihakikisha kuwa haina unyevu mwingi.
05:2606:28Funika pipa kwa kitambaa. Baada ya siku 10, mbolea minyoo ya maji maji huanza hujitengeneza. Kila siku, unaweza kukusanya lita 1 hadi 3 za mbolea minyoo.
06:2907:10Epuka kuoneza kemikali kwenye mbolea hiyo ili kuzuia vijidudu vyema kuuawa.
07:1109:35Nyunyiza mimea asubuhi mapema au jioni. Lowesha mizizi ya miche kwenye mbolea minyoo ya maji maji kabla ya kupandikiza.
09:3611:00Baada ya miezi 3 tengeneza mbolea mpya. Mbolea minyoo ya maji maji ni chanzo cha mapato.
11:0113:22Muhtasari

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *