Mbolea minyoo hutengenezwa kutoka kwa kinyesi cha minyoo.
Minyoo hutoa kinyesi wanapokula chakula. Kinyesi chao ni mbolea. Kwa vile minyoo hufa haraka, mbolea yao huwa imekithiri virutubisho. Virutubisho vilivyomo kwenye mbolea ya minyoo havibadiliki, na vinaweza kutumiwa na mimea tuu, kwa hivyo haviyeyuki udongoni.
Kutengeneza mbolea minyoo
Nyenzo zitakazotumika kutengeneza mboji hutegemea ukubwa wa uzalishaji unaohitajika. Kwa bustani za nyumbani, hata jerikani iliyokatwa upande mmoja, inaweza kutumika. Chombo hiki hujazwa na nyenzo za kikaboni.
Pata nyenzo ya kuanzia (minyoo) na kuiweka mwishoni mwa upande mmoja wa jerikan. Ongeza safu ya nyenzo kavu za kikaboni ndani ya jerikani yote, na umwagilie maji.
Minyoo huanza huzaliana huku wakikula nyenzo za kikaboni kutoka upande mmoja wa chombo hadi mwingine, wakati wakitoa kinyesi chao. Iwapo nyenzo zote za kikaboni zimetumika, ondoa mabaki ambayo ni mbolea minyoo na uongeze nyenzo mpya.
Mbolea inayozalishwa ni bora kwa mazao yote.
Mbolea minyoo ya maji maji
Maji yanayotiririka kutoka kwa mbolea ni mbolea minyoo ya maji maji (vermiwash), ambayo inaweza kutumika kama mbolea na pia ni dawa ya kuua wadudu. Mbolea minyoo ya maji maji huchanganywa na maji kwa uwiano wa 1: 1, na kuweka kwenye bomba la mgongoni na kunyunyiziwa kwenye mazao.