Rutuba ya udongo ni msingi wa uzalishaji wa mazao bora ya kilimo. Rutuba ya udongo inaweza kupunguzwa, kuongezwa au kudumishwa kulingana na shughuli mbalimbali zinazofanywa kwenye ardhi.
Kabla ya kuweka mbolea shambani, zingatia rutuba ya udongo awali, na hivyo tumia samadi, mboji na mbolea ili kuongeza rutuba ya udongo. Pia zingatia pH ya udongo, upatikanaji wa virutubisho na madini, pamoja na aina ya zao litakalopandwa.
Mbinu za Kuweka mbolea shambani
Mbolea hutoa virutubisho kwa mimea, na mbinu zinazopendekezwa ni pamoja na mbinu ya uongezaji na udumishaji, mbinu ya utoshelevu, mbinu ya uwiano wa cation (Basic Cation Saturation Ratio), na mbinu ya upimaji.
Kwanza, mbinu ya uongezaji na utunzaji hudumisha rutuba ya udongo kwa miaka ijayo na hutoa rutuba zaidi pamoja na kufidia virutubisho vinavyoondolewa. Mbinu hiyo inahusisha uwekaji wa mbolea kwa kuzingatia mahitaji ya mmea. Fosforasi na potasiamu ni bora kwa mbinu hii. Mbinu hii huonga rutuba kwenye udongo kwa muda, walakini huongeza gharama za kununua mbolea na hivyo kupunguza mapato.
Mbinu ya utoshelevu hutumiwa kukidhi mahitaji ya virutubisho vya mazao. Madhumuni yake ni kuongeza kipato katika kipindi fulani cha muda kwa kutumia kiasi kidogo cha mbolea, na kupunguza gharama. Hii hufanywa kwa kuzingatia upimaji wa udongo ili kuweka mbolea , na hivyo kuongeza madini na virutubisho kwenye udongo. Mbolea zilizopendekezwa kwa mbinu hii ni fosforasi na potasiamu.
Vile vile, mbinu ya uwiano wa cation (Basic Cation Saturation Ratio) inahusisha upatikanaji wa uwiano maalum wa cation kwenye udongo ili kupata mavuno mengi. Mbolea zinazopendekezwa kwa mbinu hii ni kalsiamu, magnesiamu na potasiamu. Uwiano wa cation unapaswa kuwa 65–85% kalsiamu, 6–12% magnesiamu na 2–5% potasiamu. Mbinu hii inafaa kwa udongo wa kichanga, kwani udongo huo hushikilia kiasi kidogo sana cha cations. Hata hivyo, mbinu hii ni bora kwa udongo wa chokaa kwani uwiano wa potasiamu ni wa juu sana katiku udongo huo.
Hatimaye ni mbinu ya upimaji huzingatia matokeo wa upimaji wa udongo kama kiasi halisi cha rutuba kinachopatikana kwenye udongo. Uwekaji wa mbolea hutegemea tofauti kati ya viwango vilivyotokea baada ya upimaji wa udongo na kiwango cha rutuba kinachohitajika kwa mazao. Hati hivyo, viwango vya upimaji wa udongo huchukuliwa kwa kukadiria.