Mahindi ni zao kuu la chakula na hunawiri katika hali ya mvua. Upandaji na utayarishaji sahihi wa shamba huhakikisha matokea zaidi.
Kina cha kupanda mahindi kinapaswa kuwa 30cm. Wakulima wanafaa kutayarisha mapema shamba ili kudhibiti magugu, mmomonyoko wa udongo na kuhimiza uotaji mzuri wa mbegu. Utayarishaji wa shamba unahusisha kuondoa vichaka, na mawe ili kurahisisha matumizi ya mashine za kilimo, trekta na mafahali.
Mbinu za maandalizi ya ardhi
Kulima kwa mikono; kunahusisha matumizi ya binadamu kulima ardhi, na kugeuza udongo ili kuulegeza pamoja na kungoa magugu.
Kutumia jembe linalovutwa na mafahali; huku kunahusisha matumizi ya mafahali waliofunzwa na wenye nguvu na afya bora. Mafahili wanapaswa kuwa na umri wa miaka 3, na uwezo wa kulima kwa kina na upana unaohitajika.
Kutumia matrekta ni njia ya haraka zaidi inayohusisha kulima, kulegeza udongo, na kupanda.
Mbinu ya kutumia dawa za kuulia magugu; njia hii inahusisha matumizi ya kinyunyizio au bomba pamoja na dawa za magugu zinazopendekezwa.
Pima uoataji wa mbegu, na kisha panda ukitumia mbegu kutoka kwa vyanzo vinavyoaminika. Panda aina moja kwa ajili ya kuota vizuri, na usafi wa aina.
Kupanda mahindi
Panda mbegu 1 kwa muachano wa 20cm ndani ya safu, na 75 au 80cm kati ya safu. Iwapo unapanda mbegu 2, tumia muachano wa 40cm ndani ya safu, na 80cm kati ya safu.
Panda asubuhi mapema kwa ukomavu sawa wa mmea.
Panda kwa mistari iliyonyooka katika muachano sahihi ukitumia kamba ili kusababisha uotaja mzuri wa mbegu.
Fuata muachano unaopendekezwa kwa aina mbalimbali za mahindi.
Panda kwenye shimo la kina cha 3cm, funika mbegu na ukanyage ili kuthibitisha udongo.