Magugu huzuia ukuaji wa miti msituni kama vile yanavyozuia ukuaji wa mazao shambani, na hivyo yanahitaji kudhibitiwa.
Magugu yanaweza kudhibitiwa msituni kwa mbinu kadhaa ambazo ni pamoja na; kukwangua na kupaka dawa, mbinu ambapo kisu kinatumika kukwangua kuzunguka gome la mti, na kisha dawa maalum hupakwa kwenye sehemu ya mti iliyokwanguliwa.
Hatua zingine za udhibiti
Mbinu ya kuondoa gome la mti kimzunguko na kupaka rangi. Kwa njia hii, gome la mti huondolewa kimzunguko kama pete, na kisha dawa maalum hupakwa kwenye sehemu ya mti iliyokwanguliwa. Unaweza pia kuamua kukata pete kuzunguka gome badala ya kuondoa gome, na kisha kupaka dawa maalum kwenye sehemu hiyo.
Kata na kupaka. Kwa mbinu hii, mti mzima hukatwa na huangushwa ardhini, na kisha dawa maalum hupakwa kwenye sehemu ya juu ya ukingo wa kisiki.
Kata na kunyunyizia dawa. Baada ya kukata mti, nyunyiza dawa kwenye sehemu ya juu ya kisiki cha mti. Hii husaidia kuhakikisha kuwa hakuna chipukizi jipya linalokua tena kutoka kwa kisiki.
Kukata na kupaka. Hapa ndipo mikato hutengenezwa kuzunguka mti, na kisha rangi maaalu hupakwa ndani ya sehemu zilizokatwa, au dawa ya kuua magugu hunyunyiziwa kwenye sehumu hizo zilizokatwa.