Nzi wa matunda ni wadudu waharibifu, ambao hushambulia sana matunda na mboga. Hii husababisha hasara kubwa kwa wakulima wa matunda na wafanyabiashara. Nzi hawa wanaweza kudhibitiwa kwa kufuata mbinu jumuishi ya kilimo.
Kutegemea aina, nzi wa matunda hutaga mayai takriban 100-1000 katika maisha yao. Wanaweza kuruka kutoka shamba moja kwenda lingine na kusababisha uharibifu mkubwa kwa wakulima. Nzi wa kike hutumia kitu kama sindano kilicho upande wa nyuma kudunga matunda na kutaga mayai mayai humu ndani. Hii husababisha madoa meusi au ya kahawia kwenye ngozi ya matunda. Baada ya siku 2, mayai huanguliwa na kugeuka kuwa maboo (minyoo myeusi). Matunda huanza kuoza na kudondoka maboo wakiendelea kukua. Baada ya wiki 1, minyoo huingia kwenye udongo, na kubadilika kuwa kifukofuko cha rangi ya kahawia. Baadaye, nzi kutoka kwenye kifukofuko na huruka.
Kutambua nzi wa matunda: Matunda huanguka kabla ya kukomaa. Unaweza pia kukagua uwepo wa nzi kwenye mitego ya nzi. Kagua shamba mara kwa mara ili kutambua uwepo wao.
Udhibiti wa nzi wa matunda
Tumia Mtego wa kunasa, ambao huvutia nzi wa matunda wa kiume na wa kike. Unaweza pia kunyunyiza mchanganyiko wa dawa za kuvutia nzi pamoja na viuatilifu ili kudhibiti nzi kutotaga mayai.
Kwa kuongezea, linda wadudu wenye manufaa kama vile koyokoyo, kwa sababu wadudu hawa hutisha nzi wa matunda. Kusanya matunda yaliyoambukizwa na uwazike ili kuzuia mabuu/ minyoo kubadilika kuwa nzi. Haribu matunda yaliyooza sokoni ili uepuke hasara.