Upandaji endelevu wa mazao pamoja na miti huongeza sana tija ya ardhi katika kipindi fulani ambacho huboresha kipato cha mkulima.
Kuchanganya mazao ya kudumu na mazao mengine au miti ni aina ya kilimo mseto, huku upandaji wa mazao ya kudumu miongoni mwa mazao mengine huongeza faida za kiuchumi na kimazingira. Mchanganyiko maalum wa mazao na miti hufanywa kulingana na mahitaji ya wakulima, mazingira na upatikanaji wa soko.
Mbinu za kilimo mseto
Kilimo mseto bora hutegemea eneo, uhusiano wa kibayolojia na upendeleo wa mkulima. Mimea ya kahawa inaweza hupandwa mseto na mboga, mimea ya viungo au matunda, pamoja na mikunde ambayo hutolea kahawa nitrojeni.
Vile vile, mimea ya kakao inaweza kupandwa pamoja na mahindi, mihogo, mipapai na migomba kwani uchaguzi wa mfumo hutegemea mapendeleo na uwezo ya mkulima. Chagua miti na mazao yanayofaa pamoja na mbinu za bora usimamizi unapoandaa mpango wa kilimo. Pia tolea zao kuu kivuli kinachotosha ili kuzuia ushindani wa mwanga, maji na virutubisho.
Zaidi ya hayo, ongeza mbolea kulingana na mahitaji ya kila zao lililopo kwenye mfumo, na dhibiti wadudu shambani. Zingatia uwepo wa vibarua na wafanyikazi mwaka mzima, na tumia mitambo ma mashine kwa ufanisi bora.Ondoa miti iliyozeeka na ile isiyozaa matunda ili kuunda nafasi zaidi katika shamba lililopo.
Mwishowe, panda mazao katika nafasi zilizoundwa kulingana upendeleo wako, na panda mazao mapya kwa mpangilio maalum kulingana na umbali sahihi unaofaa kuachwa kati ya mimea.