Ni muhimu kukausha mbegu zako vizuri. Kwa hivyo unaweza kutumia meza ambayo ina matumizi mengine zaidi.
Kukausha mpunga wakati wa msimu wa mvua inaweza kuwa shida kubwa. Tufani na mvua hufanya iwe ngumu kukausha mbegu na huathiri shamba. Kwa hivyo mbegu huharibika na haupati mavuno mazuri, unasalia tu na mbegu duni. Ili kutambua kama mbegu zimekauka vizuri, unaweza kutumia kifaa cha kupima unyevu. Pia, unaweza kuuma mbegu ili usikilize sauti ya mbegu kavu.
Kukausha vizuri
Mbegu hupata unyevu zikikaushwa moja kwa moja kwa ardhi baada ya kupura. Na hivyo, ubora wa mbegu huendelea kupungua zikipata unyevu uliyondani ya udongo.
Kwa kukaushia chini kwa sakafu, chembechembe za udongo, vumbi na takataka huchanganyika na mbegu, ambayo huathiri ubora wa mbegu hizo. Kukaushia mbegu ardhini kunahitaji kazi nyingi. Wanawake hutumia muda mwingi wa kukausha mbegu, huku wakihakikisha kwamba mpunga haujaharibiwa na watoto, kuku na mifugo wengine. Pia, kuna uwezekano wa kuchanganyisha aina tofauti za mbegu.
Kukaushia juu ya meza
Tumia meza ya mianzi ili kukukausha mpunga. Hii haitakuwa na gharama yoyote. Isipokuwa kamaba na misumari, unaweza kupata vifaa vingine katika eneo lako.
Kwa kukaushia mbegu juu ya meza, zinabaki kavu. Upepo husaidia kukausha mbegu hizo. Wakati mvua inapoanza kunyesha, unaweza kufunika mbegu kwa haraka, kwani mbegu hazitapata unyevu. Unaweza hata kukaushia mbegu zako ndani ya nyumba.
Unaweza kutumia meza kwa njia mbalimbali, kama vile kukausha samaki au mahindi, au kuitumia kama eneo la kuhifadhia. Kwa kukausha mbegu juu ya meza, wanyama wako hawawezi kufikia mbegu ili kuleta uharibifu.