Matunda ya papai yanaweza kustahimili hali za ukame na kiangazi, Papai hukuzwa sana kwa sababu ya faida zake ya kiafya, madini na virutubisho, kipato, na huhitaji ardhi kidogo.
Mahitaji ya ukuaji wa papai ni pH 5.5 hadi 7.0, joto la nyuzi 21 Celsius. Udongo wa mfinyanzi huzuia ukuaji wake, na hivyo udongo tifutifu na wa kichanga ni bora ku upandaji wa mmea. Hata hivyo papai huathiriwa na magonjwa kadhaa ambayo ni pamoja na ubwiri unga, ukungu, chule, mnyauko, uozo wa kwa shina, fundo la mizizi. Mapapai hukomaa wakati utomvu wake unapokuwa wa maji maji, na kwa hiyo unashauriwa kuvuna matunda mara kwa mara katika saa za asubuhi.
Kilimo cha mipapai
Odoa maji ya ziada kwenye ardhi. Lima ardhi ili kuandaa vitalu kwa upana wa mita 2, urefu wa sm 20 hadi 25, na muachano wa 30cm kati ya vitalu.
Pili, panda mbegu kwenye safu, na viriba vya sm10 kwa umbali wa cm 3 hadi 4. Kisha panda mbegu 2 hadi 3, lakini acha mbegu moja tu baada ya kuota ili kupunguza ushindani.
Pandikiza mwanzoni mwa mvua, na panda miche kwa kutengeneza mashimo ya upana wa sm 6o, kina cha sm60, na urefu wa sm 60cm, ukiacha umbali wa mita 2 kutoka mche mmoja hadi mwingine.
Changanya udongo na mbolea siku 15 kabla ya kupanda ili kuimarisha rutuba ya udongo. Acha muachano wa sm50 kati ya safu ili kusababisha mtiririko mzuri wa maji.
Ongeza machnganyiko wa mbolea ya kikaboni na mbolea ya madini kuzunguka miti, kwa uwiano wa 150g urea, 250g phosphate na 75g potashi na kilo 20 za samadi ya ng‘ombe kwa ukuaji sahihi wa mmea.
Mwagilia maji baada ya siku 10 hadi 20 katika majira ya baridi, na siku 6 hadi 7 katika majira ya kiangazi ili kuepuka mnyauko wa mmea. Pogoa sehemu ya juu ya mmea ili usirefuke sana.
Tunza mti 1 wa kiume kwa kila miti 15 ya kike. Dhibiti magonjwa makubwa ili kuongeza mavuno.
Ondoa magugu, hata hivyo usipalilie kwa kina kirefu. Tumia dawa za kuua magugu kabla hayajaibuka ili kuepuka kuharibu mizizi ya mimea iliyo na kina kifupi.