Kuelimisha wakulima juu ya matumizi salama ya viuatilifu kunahakikisha matumizi sahihi ya kemikali hizi, na hivyo husaidia kuboresha kanuni za kilimo.
Bila matumizi ya vituatilifu, mazao hubaki bila ulinzi na hivyo kusababisha ukuaji duni. Hata hivyo, uangalifu unapaswa kuchukuliwa wakati wa kutumia kemikali kwani zinaweza kudhuru mtumiaji na mazao. Hivyo basi, soma tahadhari kabla, wakati wa na baada ya matumizi, na pia fuatilia eneo, na andaa mipango ya dharura unapotumia kemikali.
Tahadhari za matumizi
Kwanza, soma lebo kabla ya matumizi ili kutambua kama kiuatilifu kina sumu, ni kibabuzi, kinaweza kuwaka au kulipuka. Zaidi ya hayo wakati wa kunyunyizia dawa nje, acha eneo la kutenganisha sehemu iliyotibiwa na ile ambayo haijatibiwa ili kulinda maeneo nyeti.
Zaidi ya hayo, vaa nguo za kujikinga na uzioshe baada ya kuzitumia. Pia pima vifaa utakavyotumia kabla ya kuvitumia ili kuhakikisha kuwa vinafanya kazi vizuri.
Wakati wote unaponyunyizia dawa, hakikisha una nguo za kujikinga, vifagio, sepetu na vyombo ili kujilinda dhidi ya kemikali. Tupa vyombo kwa kutumia kanuni zinazopendekezwa.
Hifadhi rekodi za viuatilifu vilivyotumika, huku ukizingatia aina, muda na mahali.
Huduma ya kwanza
Dawa ya kuua wadudu ikimezwa, daktari au wakala wa kudhibiti sumu wanapaswa kuitwa mara moja. Usichochee kutapika au kumruhusu mtu kunywa kioevu chochote.
Kwa upande mwingine kemikali inapogusana na ngozi, suuza sehemu iliyoathirika kwa maji kwa muda wa dakika 15 hadi 20. Ikiwa kemikali imevutwa mapafuni msogeze mtu kwenye hewa safi. Akiwa hapumui, tumia njia ya bandia ya kupumua.