»matumizi salama ya dawa za kuogesha mifugo (sehemu ya 2)«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=OibK3bqbzhc&t=190s

Muda: 

00:04:50
Imetengenezwa ndani: 
2013

Imetayarishwa na: 

AGRIMAT USA

Kuna aina tofauti za dawa ya kuogesha mifugo zinazotumika katika udhibiti wa kupe lakini tahadhari zinapaswa kuchukuliwa wakati wa kutumia dawa hizo ili kuepuka kusababisha uharibifu kwa watu, wanyama au mazingira.

Kemikali zinazotumiwa zaidi zimeainishwa kama organophosphates, amidines, pyrethroids za viwandani na pyrethroids za asili. Organofosfati huua kasi lakini huwa na muda mfupi wa ulinzi wa siku 2 hadi 3. Amidines kama vile amitraz na triatix zina muda uliongezwa wa ulinzi kulingana na viwango vilivyotumika. Pyrethroidi za viwandani kama decatix zina ulinzi mrefu zaidi wa siku 7 hadi 10, na pia hudhibiti wanyama dhidi ya nzi wa mbung’o. Parethroidi asilia kama vile coopers pia zinaweza kutumika.

Kuvaa nguo za kinga

Dawa inayochaguliwa inategemea idadi ya vipengele, ambavyo ni pamoja na; vifaa vinavyopatikana, bei ya dawa na ufanisi dhidi ya vimelea vingine kama vile utitiri, chawa na nzi. Liche ya dawa inayotumika, nguo za kinga kama vile ovaroli na glavu zinapaswa kuvaliwa wakati wa kushughulikia kemikali kali. Wakati wa kushughulikia organophosphates, apron ya kuzuia maji pia inashauriwa. Bidha za kutumika tayari moja kwa moja zinafaa pia zitumike kama glavu za kinga zimevaliwa.

Barakoa lazima ivaliwe ili kuzuia kuvuta kemikali.

Ushauri juu ya matumizi ya kemikali

Ikiwa kemikali yoyote (iliyokolea au iliyoyeyuka) imagusana na mwili wako, ioshe mara moja. Vyombo vyote vya kemikali vinapaswa kuwekwa mbali na watoto, na kuharibiwa vikiwa tupu.

Wauzaji wa dawa za mifugo wanaweza kutoa ushauri kuhusu dawa bora zaidi kwa hali yako, na usaidizi wa huduma zozote mbalimbali.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:30Dawa za kuogesha mifugo zinazotumiwa zimegawanywa katika makundi mbalimbali. Organofosfati, ambazo huua kasi lakini huna kipindi kifupi cha ulinzi.
00:3100:59Dawa za amidines, ambazo zina kipindi kirefu cha ulinzi kulingana na mkusanyiko uliotumiwa.
01:0001:27Dawa za Pyrethroid za viwandani, ambazo zina ulinzi mrefu zaidi wa siku 7 hadi 10, na pia zin ufanisi mzuri dhidi ya mbung‘o.
01:2801:36Dawa asili za parethroid kama vile coopers grease pia zinaweza kutumika.
01:3701:50Bidhaa itakayochaguliwa hutegemea vifaa vinavyopatikana, bei na ufanisi wazo dhidi ya vimelea vingine kama vile utitiri, chawa na nzi.
01:5102:26Bila kujali matumizi ya dawa za kuogesha mifugo, mavazi ya kinga yanapaswa kutumika.
02:2702:35Barakoa inapaswa kuvaliwa wakati wa kunyunyizia dawa
02:3602:48Kemikali yoyote ikigusana na ngozi yako, ioshe mara moja. Weka kemikali mbali na watoto.
02:4902:59Tahadhari zikifuatwa, viuatilifu havina hatari kwa watumiaji, ng‘ombe au mazingira.
03:0003:30Wauzaji wa dawa za mifugo wa ndani wanaweza kutoa ushauri kuhusu matumizi yadawa.
03:3104:50Muhtasari

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *