Nyanya hukabiliwa na magonjwa mengi na chule ni mojawapo yao. Chule husababishwa na ukungu, na inaweza kutibiwa kiasili, na kwa kutumia kemikali.
Dalili na kuzuia
Chule hujidhihirisha kwenye nyanya kama mashimo madogo yaliyo kwenye majani.
Hii huzuia mmea kugusana na udongo ulio na unyevu, ambao huhimiza ukuaji ukungu.
Epuka kumwagilia mimea maji mengi sana, na pia fanya mzunguko wa mazao. Epuka kupanda nyanya, pilipili na mbiringani mwaka kwa mwaka. Unaweza kubadilisha mazao kwa kupanda mboga za mizizi kama vile karoti na biti rut.
Udhibiti
Kwa asili, unaweza kudhibiti chule kwa kutumia mafuta ya mwarobaini, majivu na jeli ya mshubiri.
Kikemikali, unaweza kudhibiti chule kwa kutumia dawa yoyote iliyo na shaba au salfa ya kuulia ukungu, au kutumia chloro ethnyl, lakini matumizi ya kemikali yanapaswa kuwa njia ya mwisho.