Kuna makosa ambayo wafugaji hufanya katika ufugaji wa mbuzi na haya ni ghali.
Kabla ya kuanzisha ufugaji, unahitaji kuwa na maono yaani kwa nini unafuga mbuzi. Usifuge mbuzi kwa sababu watu wengine wanawafuga. Aina chotara kufugwa sana kwa sababu ya ukuaji wao wa haraka, na uzito kwa hivyo kuwahasi kunamaanisha kupoteza sifa zao nzuri. Aina safi na chotara wanaweza kujamiiana na aina wa kienyeji ili kuzalisha watoto walio na sifa zilizoboreshwa, kwa hivyo wanapaswa kuuzwa au kutumika kama wanyama wa kuzaliana.
Tahadhari katika ufugaji
Kuwa na banda la mbuzi lililoinuliwa na lenye uingizaji mzuri wa hewa ni bora. Hata hivyo, ni kosa kuwa na sakafu ya saruji ambayo hutwamisha mkojo. Mkojo huo ukichanganywa na kinyesi cha mbuzi hutoa gesi ya amonia. Gesi ya amonia husababisha mbuzi kukohoa kila wakati na kusababisha ugonjwa wa mapafu.
Usichanganye mbuzi na ng‘ombe au kondoo kwa sababu ng‘ombe na kondoo wanaweza kustahimili baadhi ya magonjwa ambayo yanaweza kuwaathiri sana mbuzi.
Tenganisha wanambuzi na majike wazima pamoja na madume ili kuzuia kuzaliana kati yao.
Kinyesi kinapaswa kuwekwa mbali na banda kwa sababu kikiwekwa karibu na banda, gesi ya amonia kutoka kwenye kinyesi na mkojo itaingia kwenye banda na kuathiri wanyama.