Maharagwe huliwa ulimwenguni kwote, na pia yanaweza kupandwa katika maeneo ya nyanda za chini. Ikiwa watu hawana ujuzi wa kutosha kuhusu mchakato wa uzalishaji, wadudu na magonjwa huwashambulia maharagwe na husababisha mavuno kidogo.
Kupanda maharagwe
Chagua mbegu ambazo hustahimili joto, ni sugu dhidi ya magonjwa, na hutoa mazao mengi. Upandaji unafaa kufanyika katika msimu wa kibaridi katika mwezi wa Novemba hadi Januari ili kupata mavuno mazuri. Kwa kuongeza, hakikisha umwagiliaji wa maji kwa maharagwe bila kutawanya maji na udongo kwa majani. Hii husababisha maua kudondoka, na kueneza magonjwa. Kudumisha rutuba ya udongo na unyevu, tumia mabaki ya mimea ili kupata mavuno mengi.
Panda katika mistari iliyo na nafasi wazi. Weka mbegu 2-3 kwa kila shimo ili kuacha nafasi ya kutosha ya kufanyia kazi. Hii husaidia kupunguza ushindani wa chakula na kuenea kwa magonjwa. Mwishowe, weka mbolea za madini ili kupata mavuno bora, na ukuaji wa haraka.