»Mafunzo ya uzalishaji wa vitunguu«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=AfZCqsEflCM&t=13s

Muda: 

02:06:03
Imetengenezwa ndani: 
2017

Imetayarishwa na: 

Ghana E-Agriculture

Vitunguu ni zao la thamani, ila kilimo chao kimeathiriwa sana na mbinu duni uzalishaji. Jambo hilo limesababisha kupungua kwa uzalishaji wa vitunguu sokoni.

Uchaguzi wa eneo; vitunguu huhitaji udongo wenye mboji, uliyo karibu na chanzo cha maji wa umwagiliaji. Utayarishaji wa ardhi: Hii lazima iwe na urefu wa 1.2 m*10, na kuinuliwa o.3m juu, pamoja na kuwekwa mbolea oza au mboji. Panda vitunguu kwenye udongo wenye unyevunyevu katika hali ya kibaridi kulingana na aina mbalimbali. Kiwango cha mbegu ni 5 – 8 kg/ha iwapo vitunguu vinapandwa moja kwa moja shambani, na 3–5 kg/ha iwapo vinapandikizwa.

Kupanda

Panda mbegu kwenye kitalu kilicho na kivuli, na uziweka kwenye jua siku 10 baada ya kuota kabla ya kuzipandikiza. Kupanda: Pandikiza vitunguu kwa umbali wa 25cm*8 cm na kina cha 3cm, vikiwa na urefu wa 10cm-15 cm. Mwagilia maji mara kwa mara. Au panda mbegu moja kwa moja kwa umbali wa 25cm*8cm.

Uwekaji wa mbolea; Weka tani 25–30 za mbolea oza kwa kila hekta. Ongeza 300kg za ammoniamu sulphate, 400kg za salfa ya potasiamu na 400kg za singo supa fosfeti au 250 – 300kg za NPK kwa uwiano wa 15:15:15 kwa kila hekta.

Sodiamu huongeza huzimiza ukuaji wa majani, fosforasi kwa ukuaji wa mizizi na potasiamu kwa kustahimili magonjwa.

Wadudu na magonjwa ya vitunguu

Hizi ni pamoja na wadudu chawa, viwavijeshi, inzi wa vitunguu na minyoo fundu.

Magonjwa ni pamoja na ukungu, ubwiri unga, virusi njano vya vitunguu, baka zambarau, uozo.

Tumia mbegu zilizothibitishwa, epuka ukusanyikaji wa maji, ukaguzi wa shamba mara kwa mara, badilisha mazao, weka kemikali, kausha mazao mapema baada ya kuvuna, na vuna ndani ya siku 140 wakati majani yanapokauka kabisa.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0001:13Uchaguzi wa eneo; vitunguu huhitaji udongo wenye mboji.
01:1401:41Utayarishaji wa ardhi: Hii lazima iwe na urefu wa 1.2 m*10m, na kuinuliwa o.3m juu.
01:4202:04Panda vitunguu kwenye udongo wenye unyevunyevu katika hali ya kibaridi
02:0502:37Vitunguu hupandwa kutimia mbegu
02:3802:56Panda mbegu na uache miche kwenye mwanga wa jua kabla ya kupandikiza.
02:5703:32Pandikiza vitunguu kwa umbali wa 25cm*8 cm
03:3304:42Changanya mboji kwenye udongo, na ongeza mbolea ya NPK.
04:4304:54Wadudu ni pamoja na wadudu chawa, viwavijeshi, inzi wa vitunguu na minyoo fundu.
04:5505:06Magonjwa ni pamoja na ukungu, ubwiri unga, virusi njano vya vitunguu, baka zambarau, uozo.
05:0705:16Tumia mbegu zilizothibitishwa
05:1705:24Fanya mzunguko wa, kagua shambamara kwa mara.
05:2505:48Weka kemikali, kausha mazao baada ya kuvuna.
05:4906:20Vuna ndani wakati majani yanapokauka kabisa.
06:2106:30Muhtasari

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *