Muhogo ni zao muhimu katika jamii nyingi barani Afrika, lakini mavuno yake kwa ujumla huwa duni. Maandalizi sahihi ya shamba ni muhimu na yanaweza kupanua mavuno mara mbili.
Mihogo inaweza kupandwa kwenye ardhi tambarare na kwenye matuta kutegemea na hali ya udongo. Hata hivyo, katika hali zote mbili za udongo, shamba linapaswa kutayarishwa vyema. Maandalizi yafanyike wakati wa kiangazi kabla ya mvua kuanza kunyesha.
Kulima na kulainisha udongolo
Ili kuandaa shamba, anza kwa kulima na kulainisha udongo. Kulima kunapaswa kufanywa kwa kina cha kutosha ili kufungua udongo vyema. Kina kinapaswa kutokuwa chini ya 15cm. Wakati wa kutayarisha shamba, ardhi inaweza kutayarishwa kama tambarare au matuta, kwa urefu wa futi moja ili kuhakikisha kwamba mizizi huendelea kukua vyema.
Suala la kuandaa ardhi tambarare au kwenye matuta linategemea na aina ya udongo. Panda mihogo kwenye shamba tambarare ikiwa udongo ni wa kichanga. Lakini kama udongo ni mzito yaani tifutifu, au mfinyanzi, panda kwenye matuta.