Kilimo mseto kinahusisha kupanda miti pamoja na mazao mengine, kwa kawaida mazao ya msimu. Miti hutoa ulinzi kwa mimea dhidi ya upepo, jua ya moja kwa moja na pia huongezeka tija.
Nyenzo zinazohitajika kwa ajili ya kuandaa ardhi kabla ya kuanzishwa shamba la kilimo mseto ni pamoja na vijiti na kamba. Ni muhimu kuchagua mbegu zenye sifa zinazohitajika kama vile upinzani dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa. Kila wakati, zingatia kiwango cha ukuaji, aina ya miti na mazao, jua linalohitajika, na rutuba ya udongo wakati wa kupanda ili kupata mpango mzuri wa kilimo mseto cha miti na mazao.
Mbinu zitakazotekelezwa
Anza kwa kufyeka vichaka na kuacha baadhi ya miti ya asili iliyopo ili kuhakikisha uanzishwaji wa kilimo mseto bora.
Kisha rundika vichaka vilivyofyekwa bila kuvichoma na uviache vioze ili kuimarisha rutuba ya udongo.
Zaidi ya hayo, lima ardhi, weka mbolea za kikaboni na uzichanganye na udongo ili kuongeza rutuba.
Baada ya hapo weka alama kwenye mahali ambapo miti na mazao vitapandwa. Chagua na panda mbegu bora zenye sifa zinazohitajika ili kuhakikisha mavuno mengi kwa kila eneo.
Hatimaye, weka nyasi kavu juu ya miche ili kuilinda dhidi ya jua ya moja kwa moja. Hakikisha uhifadhi wa unyevu wa udongo pamoja na kuimarisha rutuba ya udongo.