Unaweza kupanda lishe la hydriponic bila ya udongo, katika nafansi ndogo. Lishe la hydroponic hupandwa kwa mwaka mzima , hata katika wakati wa kiangazi.
Changamoto inao shirikishwa na kupanda lishe la kijani ni kwamba mara kadha, hakuna ardhi wa kilimo wala maji ya kutosha. Zaidi ya hayo, uzalishaji wa lishe huwa ngumu kwa mwaka mzima. Ni boro kujua kwamba, lishe huwa chakula cha wanyama kinacho pandwa kwa mbegu, na maji kidogo. Wiki moja baada ya mbegu kutoka au kuchipuka, miche wa lishe huwa na ukubwa wa takribani 30 cm.
Ulimaji wa lishe la Hydroponic.
Lishe la hydroponic hukua vyema mahali ambapo hakuna mwelekeo ziadi wa mwangaza wa jua. Kwa hivyo, ni muhimu ujenge kivuli au utumie kivuli cha chumba cha wanyama. Ni bora kuacha nafasi baina ya paa na ukutata wa chumba ili kuwezesha uingizaji wa hewa. Lishe la hydroponic humea kwenye sinia ya urefu kulingana na nusu mita, ili kuyasafirisha kwa urahisi. Na pai, lazima sinia hizo ziwe ngumu kwa kubeba uzito wa lishe. Kwa hivyo, unaweza kupanda kilo moja ya mbegu za mahindi katika sinia hizo. Ni bora kutumia sinia za plastiki kuliko za chuma kwasababu sinia za chuma huenda kutu. Chimba shimo au tundu ndogo kwenye sinia hizo, ili uwezeshe upitaji wa maji kiasi. Kisa, unaweza kujenga henga la mianzi isipo ingiza maji na mvua. Hakikisha kwamba pande moja ya henga hilo inaelekea ili kuwezesha maji kudondoka.
Unaweza kutumia mahindi, nafaka wa ngano, na mapunde tofauti kwa kutayarisha lishe. Toa mbegu zilizo vunjika na kuoza. Ongeza ndoo moja ya maji safi ya vuguvugu katika bafu lenye mbegu. Baada ya mda, toa mbegu zilizo elea juu ya maji, kwasababu hizo hazichipuki. Ili kudhibiti ukungu, weka kiganja kamili cha chumvi kwenye mbegu kwa mda wa takribani saa kumi na mbili (12). Toa mbegu zilizomea katika gunia, kisha uzitandaze kwa usawa kwenye sania. Weka sania hiyo juu ya henga la mianzi, na kama kuna hali ya kiangazi au joto, nyunyizia maji mbegu hizo kila baada ya masaa mawili, au matatu endapo kuna baridi.
Hakikisha kwamba kivuli kikavu na pia safi, ili kudhibiti ukungu. Pia, usiharibu mbegu zilizomea kwa kuzitoa kwenye sinia.
Kwa mda wa wiki moja, kilo ya mahindi huzaa kilo nane (8) za lishe. Mwisho, toa sinia , katakata lishe hilo uwape wanyama.