»Kuzidisha muhogo kwa haraka«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=sqi1Vli3Tco

Muda: 

00:05:03
Imetengenezwa ndani: 
2016

Imetayarishwa na: 

Peter Peters

Muhogo una uwiano mdogo wa kuzidisha, lakini kuzaliana kwa haraka husaidia kuongeza mavuno ya jumla ya muhogo.

Uwiano wa kuzidisha uzalishaji ni ongezeko la vipandikizi kulingana na vile vilivyopandwa. Kuzidisha kwa haraka katika muhogo hufanywa kwa kukata vipandikizi vidogo vya shina. kipandikizi kidogo cha shina ni kipande kidogo cha shina ambacho kina fundo moja au zaidi kulingana na sehemu ya shina kilichokatwa. Wakati wa kukata, tumia vifaa vikali ambavyo ni pamoja na cutlas, mkasi, na msumeno.

Vipandikizi vya shina

Shina la muhogo limegawanywa katika sehemu tatu ambazo ni pamoja na; sehemu ya mbao ngumu, sehemu ya mbao isio ngumu, na sehemu ya ncha. Vipandikizi kutoka kwenye sehemu ya mbao ngumu vinapaswa kuwa na fundo moja au mbili. Vile vya sehemu zisizo ngumu vinapaswa kuwa na urefu wa futi moja. Kwa vile vya sehemu ya ncha, ondoa majani yote lakini jihadhari usiharibu vichipukizi (vijicho), na uweke vipandikizi mara moja katika maji ili kuvizuia kunyauka.

Idadi ya vipandikizi kutoka kwenye shina moja inategemea urefu wa shina, kipenyo cha shina, umri wa mmea na hali ya hewa wakati na baada ya kupanda. Vipandikizi 60 hadi 100 vidogo vinaweza kupatikana kutoka kwa shina moja.

Matibabu ya shina

Kabla ya kupanda, tibu vipandikizi vya muhogo kwa dawa ya kuua kuvu. Fanya hivyo kwa kutumbukiza vipandikizi kwenye dawa ya kuua kuvu na viache vikauke kidogo kabla ya kupanda.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:47Muhogo una uwiano mdogo wa kuzidisha ukilinganishwa na mahindi.
00:4800:55kuzidisha kwa haraka husaidia kuongeza mavuno ya jumla ya muhogo.
005601:35Kuzidisha kwa haraka katika muhogo hufanywa kwa kukata vipandikizi vidogo vya shina
01:3602:02Wakati wa kukata, tumia vifaa vikali.
02:0303:24Vipandikizi kutoka kwenye sehemu ya mbao ngumu vinapaswa kuwa na fundo moja au mbili. Vile vya sehemu zisizo ngumu vinapaswa kuwa na urefu wa futi moja. Kwa vile vya sehemu ya ncha, ondoa majani yote.
03:2503:45Idadi ya vipandikizi kutoka kwenye shina moja inategemea urefu wa shina, kipenyo cha shina, umri wa mmea na hali ya hewa wakati na baada ya kupanda
03:4604:57Tibu vipandikizi vya muhogo kwa dawa ya kuua kuvu.

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *