Baada ya kupata vipandikizi vidogo vya shina la muhogo, tunahitaji kuviotesha kabla ya kuvipandikiza kwenye shamba kuu. Kuotesha kunaweza kufanywa kwenye kitalu au viriba.
Kuotesha vipandikizi katika viriba ni bora kwa sehemu ngumu za mashina na zile zisizo ngumu sana. Madhumuni ya kuzidisha mihogo kwa haraka ni kuzalisha vipande vya kupanda. Vipande vya kupanda vinaweza kuwa tayari miezi sita hadi saba baada ya kupandikiza.
Kuotesha Mihogo
Ili kuotesha macho (vichipukizi), chagua eneo tambarare lililokaribu na chanzo cha maji. Pima urefu na upana wa eneo. Hakikisha kwamba upana wa kitalu hukuwezesha kufikia sehemu ya kati ya kitalu kutoka pande zote mbili.
Iwapo unapanda vipandikizi vilivyo na vifundo viwili, acha umbali wa 10 kwa 10cm, na kina cha 1.5cm. Vipandikizi vinapaswa kupandwa kimlalo. Vipandikizi visivyovigumu sana vinapaswa kupandwa vikiwa vimesimama wima kwa kina ambacho ni theluthi moja ya urefu wa kipandikizi. Ncha za shina zinapaswa kuwa theluthi mbili ya urefu kipandikizi.
Vuna shina kwa urefu wa mita 1 na uzifunge kwa kifungu kilicho na vipande 50. Vijiti vinaweza kuhifadhiwa hadi wiki 8 tu. Wakati wa kuhifadhi, epuka jua ya moja kwa moja, na upepo mkali au baridi. Hakikisha kwamba vichipukizi vinaelekea juu wakati wa kuhifadhi. Vipande vya kupanda vinapaswa kuvunwa kutoka kwa mihogo yenye afya tu.