»Kuwalisha mbuzi wa maziwa«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.accessagriculture.org/dairy-goat-feeding

Muda: 

00:09:39
Imetengenezwa ndani: 
2016

Imetayarishwa na: 

Environmental Alert, DAES, KENFAP, Egerton University

Wanawake wengi barani Afrika wanapenda kuwafuga mbuzi kwa sababu ni rahisi kuwachunga hata kwenye kipande kidogo cha ardhi. Maziwa ya mbuzi huuzwa kwa bei ya juu sokoni, yana kiwango cha juu cha lishe, na pia ni mazuri kwa watoto pamoja na wazee.

Ili kutoa maziwa mengi, mbuzi wa maziwa wanahitaji kulishwa vizuri. Mbuzi waliolishwa vizuri hukua haraka na wana uwezekano mkubwa wa kuzaa watoto, pamoja na kuzalisha maziwa zaidi. Malisho husaidia kukidhi baadhi ya mahitaji ya mbuzi kama vile nguvu, protini, vitamini, na madini. Malisho ni pamoja na nyasi, mabua ya mahindi na mabaki ya mazao, majani ya ndizi, na vichaka. Mashina ya ndizi yaliyokaushwa, migrivea, majani ya viazi tamu, majani ya mbaazi, na maharagwe husaidia kuongeza uzalishaji wa maziwa. Vyanzo vingine vizuri vya protini ni pamoja na mabaki ya soya, unga wa samaki na keki ya mbegu za pamba, mabavyo mara nyingi hupatikana katika duka la vyakula vinavyonunuliwa. Lishe linapaswa kukaushwa kwa angalau siku 3 kabla ya kuwalisha mbuzi ili kuepuka kuharisha. Wape mbuzi maji safi kwa sababu maji husaidia mbuzi kumengenya lishe, na hivyo kuongeza uzalishaji wa maziwa.

Tahadhari kwa mbuzi wa maziwa

Ondoa chakula kilichobaki kutoka kwenye kihori cha chakula. Safisha vizuri kihori kabla ya kuweka chakula kingine kwa sababu mbuzi wanaweza kuwa wamekikojolea.

Chakula kinapaswa kuwekwa kwenye kihori kilichoinuliwa ili kuepuka kukichafua. Funika lishe iwapo mvua inataka kunyesha ili kibaki kavu. Epuka kuwalisha mbuzi mimea iliyo na sumu kwa sababu inaweza kusababisha uvimbe na kuua mbuzi. Changanya magadi na maji na uwape mbuzi ili kutibu uvimbe wa tumbo.

Epuka kuwalisha mbuzi vitunguu na majani ya sukumawiki kwa sababu yatasababisha maziwa kutoa harufu mbaya. Hifadhi lishe katika hali ya nyasi kavu ili kutumika wakati wa kiangazi.

Kiwango cha kuwalisha mbuzi

Wape mbuzi wa maziwa chakula kingi kadri wanapokua ili kudumisha afya nzuri. Iwapo mbuzi wana mimba, changanya chakula na mikono 3 iliyojaa lishe ya maziwa katika miezi 3 ya mwisho wa mimba ili kupata watoto wenye afya na maziwa mengi. Kwa mbuzi anayenyonyesha, ongeza mikono 3 ya lishe ya maziwa katika chakula ili kuendelea kutoa maziwa.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:45Maziwa ya mbuzi yana kiwango cha juu cha lishe, protini, na huleta mapato zaidi
00:4601:50Mbuzi waliolishwa vizuri hukua haraka na wana uwezekano mkubwa wa kuzaa watoto, pamoja na kuzalisha maziwa zaidi.
01:5103:13Baadhi ya mimea husababisha maziwa zaidi. Malisho ni pamoja na nyasi, mabua ya mahindi na mabaki ya mazao, majani ya ndizi, na vichaka
03:1404:30Lishe linapaswa kukaushwa kwa angalau siku 3 kabla ya kuwalisha mbuzi. Wape mbuzi maji yakutosha yaliyosafi .
04:3105:20Changanya magadi na maji na uwape mbuzi
05:2106:00Chakula kinapaswa kuwekwa kwenye kihori kilichoinuliwa ili kuepuka kukichafua
06:0107:10Epuka kuwalisha mbuzi mimea iliyo na sumu
07:1107:40Hifadhi lishe katika hali ya nyasi kavu ili kutumika wakati wa kiangazi.
07:4108:10Wape mbuzi wazima chakula kingi. Kwa mbuzi wana mimba, changanya chakula na mikono 3 iliyojaa lishe ya maziwa katika miezi 3 ya mwisho wa mimba ili kupata watoto wenye afya na maziwa mengi. Kwa mbuzi anayenyonyesha, ongeza mikono 3 ya lishe ya maziwa.
08:1109:39Muhtasari

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *