Mbegu za maharagwe ya soya zilizovunwa na kuhifadhiwa vibaya hupoteza uwezo wake wa kuota. Mbegu zilizo na ukungu au unyevu huoza wakati wa kuhifadhi. Kuvuna vizuri, kukausha, kupepeta, kuchambua na kuhifadhi huongeza muda wa mbegu kuishi.
Ukungu ni adui mkubwa wa maharagwe ya soya.
Kupepeta na kukausha
Vuna mbegu wakati majani yanapogeuka manjano au wakati mbegu zinapotoa sauti zinapotikiswa. Kata mimea ya soya na uyaweke kwenye virundo vidogo. Acha mirundo ya soya kwa jua kwa muda wa siku 10, na uigeuze baada ya kila siku 3, kwani hii husaidia kukausha vizuri maganda na nafaka.
Tenganisha mbegu kutoka kwa maganda kwa kuzigonga juu ya turubai safi. Walakini, usizigonge sana, kwani mbegu zitavunjika. Pepeta maharagwe ya soya ili kuondoa takataka. Chambua, na kuondoa mbegu zilizo na kasoro, ukungu, zilizoharibika, kwa sababu hazikui vizuri.
Kausha mbegu kwenye sakafu safi kwa siku 2–3. Angalia kwa makini maharage ya soya katika shamba na kwenye sehemu ya kukaushia ili kuzuia uharibifu wa wanyama. Kamwe usisafirishe mbegu kwenye mvua kwani zitapunguza ubora.
Uhifadhi
Hifadhi mbegu kwenye magunia, kwaani joto linalotokana na mbegu linaweza kupita haraka. Funga imara gunia ili kuzuia uharibifu unaotokana na panya buku au panya, nakuziweka mbali na uchafu. Walakini, usiongeze bidhaa yoyote ya kuhifadhi au kulinda mbegu kwa sababu wadudu hawawezi kupenyeza. Weka mifuko ya mbegu kwenye mbao, na uhifadhi katika chumba kilicho na hewa ya kutosha ili kuzuia unyevu unaosababisha ukungu.