»Kuunganisha/ kupandikiza miche ya embe«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.accessagriculture.org/grafting-mango-seedlings

Muda: 

00:15:25
Imetengenezwa ndani: 
2018

Imetayarishwa na: 

Practical Action, Bangladesh and Nepal, Christian Commission for Development in Bangladesh (CCDB)

Kuunganisha miche kunajumuisha kuambatanisha seheme ya juu ya mmea, ambayo hugeuka kuwa matawi na majani, kwa sehemu ya chini iliyo na mizizi mzima, ambayo hukua kama msingi wa mmea. Miche iliyounganishwa hukomaa mapema na kutoa mavuno bora ya hali ya juu.

Pandikiza / unganisha miche kabla ya msimu wa mvua ili utomvi uweze kuambatanisha sehemu ya juua na sehemu ya mizizi. Safirisha sehemu hizo za mmea kwa uangalifu, ili kuepuka uharibifu. Maembe yana vitamini nyingi, na ni chanzo cha mapato.

Kupanda sehemu ya mizizi

Chagua matunda ambayo hayajaharibiwa na uyatoe maganda. Jaza mifuko midogo na udongo wenye rutuba (mboji) kwa ukuaji mzuri wa mbegu. Weka mbegu kama upande ulioelekezwa ukiangalia juu ili kuota vizuri. Weka mifuko kwenye mahali pazuri na umwagilie maji kwa ukuaji bora. Baada ya kuota, chagua miche yenye afya tu na uweka mifuko kwenye udongo ukiacha nafasi ya kutosha kwa uunganishaji rahisi.

Utaratibu wa kuunganisha

Chagua sehemu ya juu na sehemu ya mizizi zilizo na sifa zinazohitajika kama vile kuwa sugu dhidi ya magonjwa, kutoa bidhaa sana, kuwa na kipindi kifupi cha ukuaji, na chipukikizi laini. Kata shina linalofaa la urefu wa 20cm. Kata sehemu ya juu ya urefu wa 10cm kutoka kwa shina hilo.

Kwa uunganishaji wa kabari, ambatanisha sehemu ya juu na sehemu ya mizizi iliyo na miezi 8, na kisha uzifunge na plastiki nyembamba. Kwa uunganishaji wa upande, sehemu ya mizizi ya mwaka 1 hukatwa ikiteleza/ ikipinda na kuwekwa kwenye seheme ya juu ya mche na kuziunga na plastiki nyembamba. Unaweza pia kukata matawi madogo ili kupunguza utumiaji wa virutubisho. Mara majani yanapogeuka kijani, hapo basi mimea iko tayari kuuzwa.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:43Maembe ni chanzo cha mapato na vitamini
00:4401:53Kuunganisha/Kupandikiza husababisha matunda bora ambayo hukomaa mapema.
01:5402:36Mche hugeuka kuwa mizizi na seheme ya juu ya mmea hugeuka kuwa matawi.
02:3702:43Jinsi ya kukuza sehemu ya mizizi
02:4402:48Chagua matunda ambayo hayajaharibiwa na uyatoe maganda.
02:4903:04Jaza mifuko midogo na mchanganyiko wa udongo wenye rutuba, na upanda mbegu moja.
03:0503:18Weka mifuko kwenye mahali pazuri na umwagilie maji mara kwa mara.
03:1904:34Baada miezi 3, chagua na upande miche yenye afya tu, ukiacha nafasi ya kutosha.
04:3504:44Tumia sehemu ya mizizi iliyo na miezi 8
04:4504:49Kupandikiza/ Kuunganisha hufanyika lini na jinsi gani
04:5005:27Kupandikiza kunafaa kufanywa kabla ya msimu wa mvua
05:2806:30Chagua seheme ya juu ya mmea na sehemu ya mizizi iliyo na sifa zinazohitajika.
06:3107:06Kata shina linalofaa la urefu wa 20cm, ondoa majani, na ukate vipande vya 10cm.
07:0707:40Safirisha sehemu za juu kwa uangalifu.
07:4107:45Maandalizi ya sehemu ya mizizi
07:4608:09Ondoa ncha ya mche kwa uangalifu
08:1009:41Kwa uunganishaji wa kabari, ambatanisha sehemu ya juu na sehemu ya mizizi, na kisha uzifunge na plastiki nyembamba.
09:4210:25Kwa uunganishaji wa upande, sehemu ya mizizi ya mwaka 1 hukatwa ikiteleza/ ikipinda na kuwekwa kwenye seheme ya juu ya mche na kuziunga na plastiki nyembamba.
10:2610:56Baada ya wiki 2 majani huonekana. Katika wiki 6 ondoa plastiki uliyofungisha .
10:5711:35Chimbua mimea iliyopandikizwa, uiweke kwenye kivuli na upande kwenye shamba lenye rutuba
11:3612:19Zika mimea iliyopandikizwa, kate matawi madogo kutoka kwa sehemu ya mizizi
12:2012:43Mara majani yanapogeuka kuwa mimea ya kijani, hapo inakuwa tayari kuuzwa.
12:4415:25Muhtasari.

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *