Usimamizi wa kilimo hai
Kwanza, wakulima wanapaswa kudumisha afya na rutuba ya udongo ili waweze kukuza mazao kwa mwaka mzima. Na pia wajadiliane na mamlaka za kisheria ili kuanzisha soko la bidhaa za kilimo hai ili waweze kufafanua haki na wajibu zinazohusika. Wanapaswa kuandika kanuni za soko na serikali za mitaa. Pia wanapaswa kusafisha soko kila baada ya wiki 2 na waanzishe mfumo wa dhamana ili wateja wasalimike na bidhaa zinazouzwa.
Vile vile, wekeza katika kuboresha huduma za wateja, na kupanua masoko.Tangazia wateja aina za bidhaa zilizopo na bei husika, uzito wa bidhaa, na kiasa kabla ya siku ya soko. Hatimaye, fundisha kikundi katika huduma bora za kushughulikia wateja na pia ushirikiane na taasisi mbalimbali ili kuhifadhi na kuvutia wateja.