»Kutunza sungura wachanga«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.accessagriculture.org/taking-care-young-rabbits

Muda: 

00:11:00
Imetengenezwa ndani: 
2017

Imetayarishwa na: 

Songhaï Centre

Ufugaji wa sungura unahitaji mbinu bora za uzalishaji ambazo ni pamoja na utunzaji mzuri wa sungura jike na watoto wachanga baada ya kuzaa.

Hali nzuri kwa watoto wachanga na sungura jike zinapaswa kuundwa kabla jike hajazaa tena. Sungura wachanga waliozaliwa hawapaswi kuguswa hadi siku inayofuata kwani huwa ni dhaifu, hawana manyoya wala hawafungui macho yao hadi siku 10. Watoto waliokufa wanapaswa kuondolewa kwenye kiota ili kuzuia kuenea kwa magonjwa.

Kugusa sungura wachanga kwa uangalifu

Kabla ya kugusa sungura wachanga, unafaa kusugua mikono yako na mchaichai au majani ya moringa, na uguse tumbo la mama awali. Sungura mama huwa makini sana kwa harufu, na wanaweza kuwatelekeza watoto ikiwa wamenukia harufu tofauti na yao.

Sungura wachanga wanaweza kuchukuliwa na mama mwengine ikiwa mama yao amekufa au amewatelekeza. Mama anaweza tu kuchukua watoto 2, na kila mama anapaswa kuwalisha watoto wake.

Kulisha watoto

Kiota kinapaswa kusafishwa mara kwa mara ili kuzuia pua za sungura wachanga kuziba, kwasababu huwa wanatumia pua kunusa titi za mama ili waweze kulishwa.

Baada ya siku 10–14, sungura wachanga huanza kulishwa chakula na maji. Sungura wasiyo na afya nzuri hutenganishwa na kutibiwa ili kuepusha kuenea kwa magonjwa.

Kuzalisha Sungura mama

Kipindi cha siku 35 kinapaswa kuruhusiwa kwa mama kuwalisha watoto wake kabla ya kutenganishwa ili kuwezesha kuzaliana na tija bora. Ikiwa sungura jike ni dhaifu sana subiri hadi aanze kunenepa kabla ya kuanza kuzaliana, laa sivyo watazaa sungura wachache.

Wakati sungura mama ni mjamzito, huwa hakuli vizuri na hana maziwa ya kutosha kulisha watoto wake ambao hawatakua vizuri.

Unaweza kusubiri hadi siku 28 kwa sungura wachanga 3, au siku 45 ikiwa watoto ni wengi kabla ya kuzaliana jike. Mara tu baada ya kuwaachisha kunyonya, sungura wachanga wanaweza kwenda kwenye hatua ya kunenepeshwa wakati mama anazaliana tena.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0001:18Sungura jike na watoto wachanga huhitaji utunzaji mzuri baada ya kuzaa
01:1901: 47Sungura wachanga waliozaliwa huwa dhaifu sana, na wanaweza kufa. Wanaokufa wanapaswa kuondolewa kwenye kiota.
01:4802:08Sungura mama huwa makini sana kwa harufu, kwa hivyo usiguse sungura wachanga kwa mkono.
02:0903:30Kabla ya kugusa sungura wachanga, unafaa kusugua mikono yako na mchaichai au majani ya moringa ili kuepusha sungura mama kuwatelekeza watoto
03:3104:02Watoto hulishwa mara moja kwa siku. Watoto wenye afya wana tumbo kubwa la mviringo.
04:0305:35Sungura wachanga wanaweza kuchukuliwa na mama mwengine, lakini watoto wawili tu.
05:3606:34Kiota kinapaswa kusafishwa mara kwa mara. Baada ya siku 10–14, sungura wachanga huanza kulishwa chakula na maji.
06:3507:00Sungura wasiyo na afya nzuri hutenganishwa na kutibiwa ili kuepusha kuenea kwa magonjwa.
07:0108: 40Kipindi cha kutosha kinapaswa kuruhusiwa kwa sungura mama kabla hajaanza kuzaliana tena
08:4109:30Sungura wachanga wanaweza kwenda kwenye hatua ya kunenepeshwa
09:3111:00Muhtasari

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *