»Kutumia vilima vya gunia kukuza mboga«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.accessagriculture.org/using-sack-mounds-grow-vegetables

Muda: 

00:09:30
Imetengenezwa ndani: 
2018

Imetayarishwa na: 

NOGAMU

Kwa ardhi ndogo, chakula kinaweza kuzalishwa kwa kutumia vilima vya gunia. Kufanya hivyo, changanya udongo wa juu na mbolea oza kisha uyajaze katika gunia ukiweka mawe madogo katikati. Mboga za majani hupandwa pembeni ya gunia, na mboga za kusimamishwa hupandwa juu.

Vifaa vinavyohitajika: gunia, bomba la urefu wa 1m, udongo wa juu, mbolea oza, mawe madogo, vigingi, na miche ya mboga. Changanya vipimo viwili vya mchanga na kipimo kimoja cha mbolea oza. Jaza gunia na mchanganyiko huo hadi 15 cm. Weka bomba (pipe) katikati na uijaze na mawe madogo. Jaza eneo iliyokaribu na bomba na mchanganyiko wa udongo na mbolea. Chomoa bomba gunia litakapojaa. Imarisha gunia katika mahali moja kwa kutumia vigingi, na ukate mashimo madogo ya 2cm ukiacha nafasi ya 10cm baina ya mashimo haya. Mwagilia maji vizuri na upande juu ya gunia mboga zinazohitaji kusimamishwa, na mboga za majani zipandwe pembeni. kisha mwagilia maji baadae.

kurutubisha udongo

Tumia virutubisho asili vya mimea vilivyotengenezwa kwa kujaza chombo hadi robo tatu na majani mbichi yaliyokatwa. Ongeza maji, na ukoroge mara moja kila siku kwa siku 5. Nyunyiza mara moja kila wiki 2 kwa kuchanganya theluthi moja ya virutubisho asili vya mimea na theluthi tatu ya maji.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:50Kwa ardhi ndogo, chakula kinaweza kuzalishwa kwa kutumia vilima vya gunia
00:5101:10Jinsi ya kuandaa kilima cha gunia na kutunza rutuba ya udongo.
01:1101:48Vifaa vinavyohitajika: gunia, bomba la urefu wa 1m, udongo wa juu, mbolea oza, mawe madogo, vigingi, na miche ya mboga.
01:4902:25Andaa kilima cha gunia katika mahali palipo na mwangaza wa jua, na kivuli.
02:2602:47Changanya vipimo viwili vya mchanga na kipimo kimoja cha mbolea oza
02:4802:59Jaza gunia na mchanganyiko huo hadi 15 cm.
03:0003:29Weka bomba (pipe) katikati na uijaze na mawe madogo
03:3003:52Jaza eneo iliyokaribu na bomba na mchanganyiko wa udongo na mbolea
03:5304:08Chomoa bomba gunia litakapojaa.
04:0904:23Imarisha gunia katika mahali moja kwa kutumia vigingi
04:2404:54Kata mashimo madogo ya 2cm ukiacha nafasi ya 10cm baina ya mashimo haya.
04:5505:29Mwagilia maji vizuri
05:3005:46Panda juu ya gunia mboga zinazohitaji kusimamishwa, na mboga za majani zipandwe pembeni.
05:4706:14Mwagilia maji kila siku baada ya kupanda, na mara mbili baada ya kustawi.
06:1506:41Tumia virutubisho asili vya mimea vilivyotengenezwa ili kudumisha rutuba ya udongo.
06:4206:48Jaza chombo hadi robo tatu na majani mbichi yaliyokatwa. Ongeza maji kwa kujaza chombo.
06:4906:52Koroga mara moja kila siku kwa siku 5.
06:5307:01Changanya theluthi moja ya virutubisho asili vya mimea na theluthi mbili za maji.
07:0207:17Nyunyiza mchanganyiko mimea mara moja kila wiki 2.

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *