Viwango vya juu vya unyevu husababisha uozo wa viazi, na hivyo kufanya utunzaji wa viazi kuwa mgumu. Kutoa joto baridi kwa kutumia machujo kunaweza kuhifadhi viazi kwa muda wa takribani miezi 6.
Vuna viazi katika siku 90 wakati vimekomaa, na uvifunike wakati wa kuvisafirisha kwa eneo la kuvichagua. Hii husaidia kuepuka mwanga wa jua ambao unaweza kusababisha viazi kubadilika kuwa rangi ya kijani. Safisha mikono na utenganishe viazi vilivyoharibika na viliyoathiriwa ili kuzuia kueneza uharibifu. Hakikisha kwamba chumba cha kuhifadhia kinaruhusu mzunguko wa hewa na upenyezaji wa mwangaza ili kuhifadhi viazi poa. Pia machujo kwenye sakafu ya chumba cha kuhifadhia, na uyamwagilie maji. Sakafu hutengenezwa kwa saruji, mchanga uliyosindiliwa, au mbao.
Hatari ya unyevu
Kagua kiwango cha unyevu kilicho ndani machujo ukitumia vidole. Tandaza viazi juu ya machujo yaliyo na unyevu, na uvifunike kwa safu nyingine ya machujo. Kisha tandaza viazi vingine juu. Unaweza kuongeza hadi safu 5 za viazi ili kurahisisha mchakato wa kukagua safu ya chini. Kagua viazi kila wiki ili kuhakikisha kwamba havijaharibika, lakini usiongeze maji. Safirisha viazi sokoni ukitumia magunia, mifuko ya plastiki iliyotobolewa, na vikapu.