»Kutumia chambo cha chakula kuua nzi wa matunda«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.accessagriculture.org/killing-fruit-flies-food-baits

Muda: 

00:12:20
Imetengenezwa ndani: 
2017

Imetayarishwa na: 

Agro-Insight

Nzi wa matunda ni moja wapo ya wadudu ambao huharibu sana matunda ulimwenguni kwote. Hata hivyo, teknolojia zaidi zimebuniwa kupunguza tatizo hilo.

Nzi hao husababisha uharibifu kubwa katika matunda kwa kutaga mayai yao ndani ya ngozi ya matuda. Mayai hayo yanapoanguliwa, mabuu (minyoo myeupe) ambayo hotokea husababisha uozo. vyambo vinavyotumiwa kudhibiti nzi wa matunda ni pamoja na: chakula kilicho na protini nyingi, na sukari ambavyo huhitajika kwa nzi ili waweze kustawi, kukua na kutaga mayai. Nzi wa matunda wanaweza kunusa chakula kutoka umbali wa mita 10. Baadhi ya vyambo vya kununuliwa huwa na harufu inayoweza kuwavutia nzi kutoka umbali mkubwa zaidi. Tumia chambo cha kununuliwa kilichochanganywa na dawa ya kuua wadudu.

Mitego ya pheromone (harufu za hisia za wadudu)

Chambo hutumiwa kama dawa ya kunyunyiza. Walakini, tumia mitego ya pheromone kukagua uwepo wa nzi. Nzi huonekana maembe yakiwa na upana wa 3m. Mara baada ya kugunduliwa, changanya maji na chambo kwa uwiano wa lita 3:1. Rekebisha tundu la mrija wa kunyunyizia na unyunyize dawa katika upande wa juu na chini ya majani kwa kila mti, na kwa upana wa mita 1 kwa 1. Dawa hufanya kazi kwa angalau siku 10 baada ya kunyunyizwa. Usinyunyize dawa siku iliyo na upepo. Nyunyiza tena bada ya mvua kubwa. Nyunyiza asubuhi wakati nzi huwa na shughuli sana.

Kulinda chambo dhidi ya mvua

Kata chombo cha manjano kati kati kisha upake chambo kinachonata ndani yake. Ninginiza chombo kwenye mti upande uliyokatwa ukiangalia chini ili kuzuia chambo kunyeshewa na mvua. Loweka sponji kwenye chambo cha chakula, na uifungie chini ya kifuniko ili isinyeshewe. Ninginiza sponji hii kwenye mti. Tumia mbinu nyingine za kudhibiti nzi pamoja na chambo cha chakula. Mbinu hizi ni pamoja na ; kuokota na kuharibu matunda yaliyoanguka, na kuhimiza uwepo wa madui asili wa nzi kama vile koyokoyo. Chambo hakiui wachavushaji wa mbegu za maua.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:55Nzi hutaga mayai yao ndani ya ngozi ya matuda. Mayai hayo yanapoanguliwa, mabuu (minyoo myeupe) ambayo hotokea husababisha uozo
00:5602:39Chambo hutumiwa kudhibiti nzi wa matunda ni pamoja na: chakula kilicho na protini nyingi, na sukari
02:4003:09Baadhi ya vyambo vya kununuliwa huwa na harufu inayoweza kuwavutia nzi kutoka umbali mkubwa zaidi
03:1003:45Tumia mitego ya pheromone kukagua uwepo wa nzi.
03:4604:02Kagua mitego kwa uwepo wa nzi wa matunda kabla ya kunyunyizia dawa.
04:0304:59Rekebisha tundu la mrija wako wa kunyunyizia ukutumia maji.
05:0005:24Changanya maji na chambo kwa uwiano wa lita 3: 1.
05:2506:23Nyunyiza dawa katika pande zote mbili za majani kwa kila mti, na kwa upana wa mita 1 kwa 1.
06:2407:39Dawa hufanya kazi kwa angalau siku 10 baada ya kunyunyizwa. Usinyunyize dawa siku iliyo na upepo. Nyunyiza tena bada ya mvua kubwa. Nyunyiza asubuhi.
07:4009:03Linda chambo cha chakula dhidi ya mvua.
09:0409:41Tumia mbinu nyingine za kudhibiti nzi pamoja na chambo cha chakula.
09:4210:10Sababu ya kutumia chambo cha chakula kuliko mbinu nyingine. Vyambo vya chakula haviui wachavushaji wa mbegu za maua.
10:1112:20Muhtasari

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *