Chukua masega yako na kuyaponda kwa kutumia mikono yako ili kutoa asali na chuja asali kwa ili kutenganisha asali na masega.
Asali hii si nzuri kwa matumizi ya binadamu kwani huwa imekaa kwenye mzinga kwa muda mrefu. Baada ya kuchuja acha masega kwa siku kadhaa ili kuwezesha nyuki kuyasafisha, na kisha chukua masega na uyachemshe. Kisha tumia chujio kutenganisha nta kutoka kwa takataka na uitupe. Tutakuwa na nta iliyoimarishwa baada ya kupoa, na kisha safisha chujio ili hurahisisha mchakato unaofuata. Kata nta katika vipande na kuiweka kwenye kitambaa cha karatasi mbili na kisha juu ya sufuria.
Kuchemsha nta
Ingiza nta ndani ya oveni na uweke karatasi ya alumini chini yake. Nta huyeyuka kupitia makaratasi. Usitupe karatasi hizo kwani zinaweza kutumika tena. Nta huachwa kwa muda kadhaa ili ibadilike kuwa ngumu, na kisha nta hutenganishwa kwa maji.
Matumizi ya nta
Nta hupakwa ndani ya ubao wa mzinga wa nyuki ili kuwahimiza nyuki kujenga juu yake. Nta pia zinaweza kufinyangwa ili kutumika kutengeneza vitu kama vile mishumaa. Hata hivyo, kuwa mwangalifu endapo unatekeleza mchakato huo kwa kuwa nta zinaweza kuwaka moto sana hasa ikiwa unatumia mfumo wa bunsenbana.