Ulimwenguni kwote Pilipili hutumika kuongeza ladha kwenye vyakula. Kutengeneza pilipili iliyosagwa ni njia nzuri ya kupata pesa kwa muda mfupi.
Ili kutengeneza pilipili iliyosagwa iliyo na ubora wa juu, tumia aina moja pekee ya pilipili. Pilipili hii ni vizuri kuvunwa bila mashina.
Usafi wakati wote
Safisha pilipili na kuondoa zilizooza na zilizoharibika. Kausha pilipili vizuri ukitumia eneo la kukausha la gesi, au jua kwa siku 5–10. Ingawa pilipili zinatoka sokoni, zichambue, zisafisha na uzikaushe tena.
Ili kuzipa ladha nzuri na harufu ya kuvutia, ongeza viungo kama chumvi, tangawizi iliyokauswa, na vitunguu saumu. Chumvi huongeza ladha na pia kuhifadhi pilipili. Saga pilipili na viungo vingine kwenye kinu safi ili upate unga laini.
Baada ya kuisaga pilipili, acha ipoe kabla ya kuiweka kwenye chupa safi kavu. Iwapo utatumia chupa zilizotumika awali, safisha na sabuni, maji, na dawa ya klorini. Dumisha usafi wakati wote.
Weka alama inayoonyesha jina maalum la bidhaa na tarehe ya mwisiho wa kutumia pilipili hiyo.