Unga wa ndizi hutayarishwa kutoka kenye ndizi mbichi zilizovunwa au kununuliwa. Unga wa ndizi unaweza kuishi kwa muda bila kuharibika kuliko ndizi mbichi, na unaweza kutumika kwa njia nyingi. Bei nzuri inaweza kupatikana na unga huo.
Unga wa ndizi hutumika kwa bidhaa kama vile uji, chapati, keki na ugali.
Jinsi ya kutayarisha unga wa ndizi
Vuna ndizi au nunua tu. Osha ndizi ili kuondoa uchafu wowote.
Katakata ndizi kwa vipande vidogo. Usiondoe maganda ili usipoteze virutubishi.
Kausha vipande hivyo katika eneo la kukaushia kwa siku 3 hadi 5. Kuwa makini na kudumisha usafi.
Pindua vipade vilivyo katwakatwa kila siku ili vikauke vizuri, hadi vitakapopasuka kwa urahisi.
Kusanya na uchukue vipande vilivyokaushwa kwa mashini ya kusaga, na uvisage kwa unga.
Kujaza na kuhifadhi
Pakia unga kwenye mifuko au vyombo visivyopenyeza hewa.
Hifadhi unga huo katika mahali pakavu. Unga wa ndizi unaweza kuishi kwa muda bila kuhariba kuliko ndizi kavu.
Vipimo kwa kiwango kinachohitajika na wateja vinaweza kufanywa.
Unga wa ndizi una manufaa nyingi kama vile virutubishi na fedha.