Karanga za shea ni chanzo kikubwa cha mapato, na hutumiwa zinapochakatwa kuwa siagi ya shea. Zinapochakatwa vizuri, huwa zinatoa bidhaa kadhaa kama vile mishumaa na sabuni.
Kupata siagi ya shea yenye ubora huanza kwa kukusanya matunda shambani katika wakati sahihi, ili yasitokeze ukungu na wala kuota.
Usindikaji
Anza kwa kukusanya matunda na kuondoa karanga ili kuzuia matunda kutokeza ukungu na kuota.
Kisha tokosa karanga kwa muda wa dakika 30 ili kupunguza kiwango cha mafuta kilichomu.
Tandaza karanga kwenye ardhi safi ili ziweze kukauka vyema. Karanga zilizokaushwa vyema hupasuka.
Chambua na tenganisha maganda ya karanga kutoka kwa punje, na ukaushe tena.
Tenganisha karanga nzuri kutoka kwa karanga mbaya ili kupata bidhaa bora. Karanga mbaya zinaweza kutumika kutengeneza mishumaa na sabuni.
Ponda karanga katika vipande vidogo na kaanga.
Kisha saga karanga ukitumia kinu, jiwe la kusaga au mashine na changanya kwa mkono. Ongeza maji na endelea kuchanganya hadi siagi itengane.
Mwishowe chemsha mafuta yaliyotenganishwa, mimina siagi safi iliyo juu na acha ipoe.